KOREA KASKAZINI-KOREA KUSINI-USALAMA

Askari wa Korea Kaskazini apigwa risasi akijaribu kutoroka

Eneo la linalotenganisha Korea Kaskazini na Korea Kusini (DMZ) , (hapa ni upande wa Korea Kusini).
Eneo la linalotenganisha Korea Kaskazini na Korea Kusini (DMZ) , (hapa ni upande wa Korea Kusini). Kèoprasith Souvannavong / RFI

Askari wa Korea Kaskazini amepigwa risasi akijaribu kutorokea Korea Kusini. Tukio hilo limetokea Jumatatu hii mchana katika eneo linalotenganisha Korea hizo mbili. Askari huyo alijeruhiwa na risasi zilizofyatuliwa kutoka upande wa Korea Kaskazini.

Matangazo ya kibiashara

Jeshi la Korea Kusini limeongeza kiwango cha chake cha tahadhari, kwa kutarajia uwezekano wa uchokozi wa Korea Kaskazini.

Jaribio hili la kutoroka limewashangaza wengi wakati ambapo eneo hilo la mpakani la Panmunjeom ni lenye ulinzi mkubwa. eneo hili ndilo linalotenganisha Korea mbili, ambapo askari wa Korea Kusini na wale wa Korea Kaskazini wanakaribina uso kwa uso wakiwa na silaha zao mikononi.

Kwa mujibu wa jeshi la Korea Kusini, askari huyo mtoro aliondoka eneo lake alipokua akitoa ulinzi mapem amchana na taarifa ya kupotea kwake ilitolewa na wenzake na hapo ndipo walianza kumfyatulia risase akijaribu kukimbilia Korea Kusini. Alijeruhiwa pegani na mkononi. Aliokotwa mita 50 kutoka mpakani na askari wa Korea Kusini na alisafirishwa kwa helikopta hadi hospitalini.

Pamoja na mvutano kati ya nchi hizi mbili, eneo linalotenganisha Korea mbili limekua likitembelewa na watalii wengi kutoka nchi za kigen, wakivutiwa na eneo ambalo linachukuliwa kama moja ya ya maeneo maarufu ya vita vya baridi.