MAREKANI-UFILIPINO-USHIRIKIANO

Trump: Nina uhusiano mzuri na Durtete

Mazungumzo kati ya Rais wa Marekani Donald Trump na mwenzake wa Ufilipino Rodrigo Duterte, Novemba 12, 2017.
Mazungumzo kati ya Rais wa Marekani Donald Trump na mwenzake wa Ufilipino Rodrigo Duterte, Novemba 12, 2017. REUTERS/Jonathan Ernst

Rais wa Marekani Donald Trump amekutana na Rais wa Ufilipino na kubaini kwamba ana “uhusiano mzuri na kiongozi wa Ufilipino Rodrigo Durtete” wakati wa ziara yake barani Asia.

Matangazo ya kibiashara

Utawala wa uliopita wa Barack Obama ulimshutumu mara kadhaa Rais Durtete kuhusu vita vyake dhidi ya mihadarati ambavyo vimesababisha vifo vya watu 4000.

Haijabainika iwapo Trump alizungumza kuhusu ukiukaji mkubwa wa haki za kibinaadamu nchini humo licha ya shinikizo za yeye kufanya hivyo.

Baada ya mkutano wa faragha kati ya viongozi hawa wawili, rais Trump hakujibu kuhusu iwapo alizungumzia kuhusu ukiukaji wa haki za kibinaadamu. Bw. Durtete, kupitia msemaji wake, amesem akuwa suala la haki za binadamu halijazungumziwa katika mkutano wao.

Hata hivyo msemaji wa Wahite House, Sarah Sanders, amebaini kwamba suala hilo lilijadiliwa kwa ufupi na wawili ho hususan katika vita dhidi ya mihadarati lakini hakutoa maelezo zaidi.