MAREKANI-KOREA KUSINI-KOREA KASKAZINI-USALAMA

Seoul na Washington waendesha mazoezi makubwa ya kijeshi

Manowari za Marekani zikiwa pamoja na zile za Korea Kusini katika bahari ya Pasifiki kati ya Japani na rasi ya Korea Novemba 12, 2017.
Manowari za Marekani zikiwa pamoja na zile za Korea Kusini katika bahari ya Pasifiki kati ya Japani na rasi ya Korea Novemba 12, 2017. Courtesy Aaron B. Hicks/U.S. Navy/Handout via REUTERS

Majeshi ya Marekani na Korea Kusini yanafanya mazoezi makubwa ya pamoja katika bahari ilio kati ya Japan na rasi ya Korea. Mazoezi haya yalianza tangu mwishoni mwa juma lililopita. Mazoezi ambayo yanaendeshwa na vikosi vya wanaanga kutoka nchi hizi mbili.

Matangazo ya kibiashara

Viongozi wa Korea Kaskazini wanasema mazoezi kati ya Korea Kusini na Marekani yanalenga Korea Kaskazini, ambapo mpango wake wa nyuklia unaangaziwa katika ziara ya Rais wa Marekani Donald Trump barani Asia, ziara ambayo anahitimisha Jumanne hii.

Ndege tatu kubwa za kijeshi, manowari 11 za Marekani, helikopta 7 za Korea Kusini vinatumiwa katika mazoezi haya makubwa ambayo hayajawahi kufanyika tangu miaka kumi iliyopita. Mara ya mwisho ndege hizi tatu zilitumiwa katika mazoezi kama haya miaka kumi iliyopita katika kisiwa cha Guam katika bahari ya Pasifiki.

Kwa mujibu wa wadadisi wa mambo operesheni hii inaendana na uwezekano wa mashambulizi kwenye miundombinu ya Korea Kaskazini.

Lengo ni kuonyesha uwezo wa nchi hizi mbili washirika dhidi ya Pyongyang ambayo imeongeza harakati zake za kurusha makombora ya masafa marefu na kuendelea na mpango wake wa nyuklia. Pia haya ni mazoezi ya kwanza ya pamoja tangu Seoul na Washington walitangaza mnamo mwezi Oktoba kuongeza silaha muhimu za Marekani katika rasi ya Korea

Siku ya Jumatatu Novemba 13, Pyongyang ilishtumu mazoezi haya, katika barua iliyotumwa kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa. Pyongyang inayachukulia mazoezi haya kama uchokozi na kuishtumu Marekani kutaka "kusababisha maafa makubwa ya binadamu.