UTURUKI-USALAMA-SIASA

Walimu 107 watafutwa kwa kuwa na uhusiano na Gulen Uturuki

Kiongozi wa Uturuki Tayyip Erdogan.
Kiongozi wa Uturuki Tayyip Erdogan. REUTERS/Umit Bektas

Serikali ya Uturukiimetoa Jumatatu hii waranti wa kukamatwa kwa walimu 107 kwa madai ya kuwa na uhusiano na kiongozi wa kidini alie uhamishoni, Fethullah Gülen, ambaye Ankara inamshtumu kuchochea jaribio la mapinduzi lililotibuliwa mwezi Julai 2016, shirika la habari la Uturuki, Dogan, limearifu.

Matangazo ya kibiashara

Walimu hamsini na mmoja walikamatwa katika mji wa Ankara, Dogan limeaandika, likiongezea kuwa operesheni inaendelea kuwaweka nguvuni wengine.

Walimu hawa walikuwa wamesimamishwa kazi katika operesheni ya kamata kamata iliyofuata baada ya jaribio kushindwa, shirika hilo lilisema.

Watu zaidi ya watu 50,000 wamewekwa kizuizi kwa kusubiri kuhukumiwa kwa shutma ya kujaribu au kuungana moja kwa moja na jaribio hilo, na watumishi wa umma 150,000, walimu au wanajeshi wamefukuzwa au kusimamishwa kazi tangu mwezi Julai 2016.

Fethullah Gülen anachukuliwa na Uturuki kama adui wao nambari moja. Bw Gulen yuko uhamishoni nchini Marekani.