MAREKANI-KOREA KASKAZINI-VIKWAZO

Marekani yaiwekea vikwazo vipya Korea Kaskazini

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un katika mkutano wa ofisi ya kisiasa ya Chama cha tawala kwenye picha ya KCNA.
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un katika mkutano wa ofisi ya kisiasa ya Chama cha tawala kwenye picha ya KCNA. KCNA via REUTERS

Marekani imeamua kuweka vikwazo vipya dhidi ya Korea Kaskazini. Uamuzi huo ulichukuliwa siku ya Jumanne, Novemba 21. Tangazo kuhusu vikwazo hivyo lilitolewa siku moja baada ya tangazo la Donald Trump, ambaye alishtumu nchini zinazounga mkono ugaidi.

Matangazo ya kibiashara

Marekani imeamua kuimarisha shinikizo dhidi ya matarajio ya nyuklia ya Pyongyang.

"Tumeamua kuimarisha shinikizo la kiuchumi kwa Korea Kaskazini ili kuitenganisha na vyanzo vya nje vya mapato," Waziri wa Fedha wa Marekani alisema katika taarifa yake kuhusu vikwazo hivyo.

Kwa jumla, makampuni kumi na tatu yanalengwa na vikwazo hiyo, ikiwa ni pamoja na makampuni nne ya China. Makampuni haya ya China yanahusika na kuagiza na kusafirisha kuelekea Korea Kaskazini makaa ya mawe na chuma, au vifaa vinavyohusiana na mitambo ya nyuklia kwa mujibu wa Wizara ya Fedha ya Marekani. Moja ya makampuni yanayolengwa imekua ikisafirisha wafanyakazi wa Korea Kaskazini kwenda China, Urusi, Cambodia na Poland.

Marekani pia imelenga mashirika na makampuni ya Korea Kaskazini yanayojikita katika sekta ya uchukuzi wa majini. Meli ishirini zinazotuhumiwa kukiuka vikwazo vilivyowekwa na Baraza la Usalama, zimewekewa vikwazo.

Vikwazo hivi vipya ni sehemu ya agizo lililosainiwa mnamo mwezi Septemba na Donald Trump, vikwanzo ambavyo vinaadhibu kampuni yoyote ambayo ina uhusiano wa biashara na Pyongyang.