Pakistan

Serikali ya Pakistan yaomba msaada wa jeshi baada kuzuka vurugu dhidi ya maandamano ya Waislam

Waandamanaji wa kiislam nwakabiliana na polisi katika njia panda ya  Faizabad huko Islamabad, Pakistan November 25, 2017. REUTERS/Stringer
Waandamanaji wa kiislam nwakabiliana na polisi katika njia panda ya Faizabad huko Islamabad, Pakistan November 25, 2017. REUTERS/Stringer © Reuters

Serikali ya Pakistani imetoa wito kwa jeshi lenye nguvu la nchi hiyo kupeleka askari katika mji mkuu Islamabad jana Jumamosi baada ya machafuko ya mauti kuzuka wakati polisi walipojaribu kuwatawanya maandamano ya waislamu ambayo yamezorotesha shughuli za mji kwa majuma kadhaa.

Matangazo ya kibiashara

Takribani watu sita wameuawa na 190 wamejeruhiwa 137 kati yao ni wafanyakazi wa usalama katika mapigano makali wakati polisi waklijaribu kutawanya waandamanaji mapema jana Jumamosi.

Hata hivyo hii leo Jumapili hali imekuwa ya mvutano baada ya jaribio la kuwatawanya waandamanaji kutumbukia katika ghasia huku jeshi likionekana kusita kuitikia mwito wa serikali kusaidia kutuliza hali ya mambo.

Mamia kwa maelfu ya waandamanaji bado wameendelea kukaa katika barabara na njia panda zinazounganisha mji mkuu Islamabad na miji jirani ya Rawalpindi huku waandamanaji jana usiku wakituma video mtandaoni ya maombi ya maziko yanayofanyika katika eneo walilojikusanya.