BURMA-PAPA FRANCIS-USALAMA

Papa Francis azuru Burma

Katika mji wa Rangoon, mji mkuu wa Burma, kiongozi wa Wabuddha apita karibu na bango lililo na pich ya Papa Francis, ambaye anataraji kuzuru nchi hiyo leo Jumatatu Novemba 27, 2017.
Katika mji wa Rangoon, mji mkuu wa Burma, kiongozi wa Wabuddha apita karibu na bango lililo na pich ya Papa Francis, ambaye anataraji kuzuru nchi hiyo leo Jumatatu Novemba 27, 2017. REUTERS/Jorge Silva

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Papa Francis anaanza leo Jumatatu, Novemba 27, ziara ya siku nne nchini Burma kabla ya kusafiri kuelekea nchi jirani ya Bangladesh. Hii ni mara ya kwanza Papa Francis kuzuru nchi ya Burma.

Matangazo ya kibiashara

Ziara hii itamruhusu kutembelea jamii ya watu wachache Wakatoliki katika kanda hiyo, lakini ziara hiyo hasa ni katika hali ya kutafutia suluhu mgogoro wa jamii ya Waislamu wachache wa Rohingya.

Ziara hii ya kiongozi wa Kanisa Katoliki nchini Burma ni katika hali ya kutafutia ufumbuzi mgogoro wa kibinadamu wa Rohingyas uliosababishwa na ukandamizaji wa jeshi la Burma. Hali hiyo ilisababisha Waislamu wengi kutoka jamii hiyo kukimbilia katika nchi jirani ya Bangladesh.

Katika mji wa Rangoon, Papa Francis atatoa wito kwa kudumisha amani na ushirikiano wa amani na jamii za watu wa wachache.

Nchini Bangladesh kuna wakimbizi zaidi ya 600,000 kutoka jamii ya Rohingya ambao wameendelea kukabiliwa na mvua na maporomoko ya udongo. Na kurejea kwao nchini ni vigumu licha ya makubaliano ya hivi karibuni kati ya Burma na Bangladesh.

Papa Francis atakutana kwa mazungumzo na Mkuu wa jeshi la Burma. Licha ya ufunguzi wa mchakato wa kidemokrasia, Mkuu wa majeshi ya Burma bado ana uwezo mkubwa, hali ambayo inapunguza mamlaka ya Aung San Suu Kyi.

Bi Aung San Suu Kyi ambaye amekua akikosolewa kwa ukimya wake kuhusu hatma ya Waislamu wa jamii ya Rohinga atakutana na Papa Francis, ambaye anakuja kumuunga mkono nchini kwake.

Wakatoliki wa Burma wamsubiri Papa

Burma ina Wakatoliki 650,000, sawa na 1.2% ya idadi ya watu waishio nchini humo. Maelfu ya watu hao walisafiri katika mji wa Rangoon kukutana na Papa Francis.