INDONESIA-HALI YA HEWA

Watu 100,000 kuhamishwa kufutia volkano Bali, Indonesia

Mlima wa volkano, Bali, Novemba 26, 2017.
Mlima wa volkano, Bali, Novemba 26, 2017. Antara Foto/Nyoman Budhiana/ via REUTERS

Serikali ya Indonesia inatarajia kuwaondoa hadi watu 100, 000 karibu na mlima mkubwa wa Volcano wa Bali. Mapema asubuhi, mamlaka imetangaza tena hali ya tahadhari karibu na mlima wa volkano wa Agung katika eneo la Bali.

Matangazo ya kibiashara

Kwa wiki moja sasa, moshi umekua ukitokea katika mlima wa volcano Agung, ambao unatishia kulipuka. Wakazi wanaoishi kilomita 10 ya eneo hilo wameagizwa kuhama na uwanja wa ndege wa Bali umefungwa kwa muda wa saa 24.

Majivu na moshi wa Volcano hiyo imefikia urefu wa zaidi ya mita 3000 juu ya mlima huo hali iliyosababisha giza.

Maafisa wamehimiza na kuwasaidia maelfu ya wakaazi na watalii kulihama eneo hilo na kwenda kwingine.

Mwishoni mwa mwezi Septemba, mamlaka ilitangaza hali ya tahadhari kubwa na watu 150,000 walilazimika kuyahama makazi yao upande wa mashariki mwa Bali. Kutokuwepo kwa mlipuko, hali ya tahadhari ilishuka na idadi kubwa ya watu ilirudi nyumbani.

Kulingana na mlipuko wa volkano wa mwaka 1963 ambao uliuawa watu 1,500, wataalam wa masuala ya volkano wanatabiri kuwa moshi na majivu vinaweza kudumu mwezi mmoja kabla ya mlima huo wa volcano kuanza kulipuka kwa kiwango kikubwa.