BURMA-EU-HAKI

Umoja wa Ulaya wataka haki sawa nchini Burma

Waislamu kutoka jamii ya Rohingya katika kambi ya Cox' Bazar, Bangladesh.
Waislamu kutoka jamii ya Rohingya katika kambi ya Cox' Bazar, Bangladesh. REUTERS/Navesh Chitrakar

Umoja wa Ulaya umeitaka Burma kuheshimu haki za binadamu na kutenga baadhi ya jamii katika masuala ya kuliendelea za taifa hilo. Hayo yanajiri wakati ambapo Burma inaendelea kushtumiwa kutowatendea haki Waislamu kutoka jamii ya Rohingya

Matangazo ya kibiashara

"Haki sawa" inapaswa kuheshimshwa katika jimbo la Akaran ili kuruhusu kurudi kwa wakimbizi 620,000 wa Rohingya waliokimbilia nchini Bangladesh, amesema Alhamisi Kristian Schmidt, balozi mpya wa Umoja wa Ulaya nchini Burma.

"Kipaumbele cha kwanza kwa serikali za mitaa na serikali kuu ya Burma ni kuanzishwa kwa utawala wa sheria, kuanzishwa utawala wa kiraia usio na ubaguzi (...) na haki sawa kwa wote," Kristian Schmidt amebaini katika mahojiano na shirika la habari la Reuters mjini Rangoon.

"Sababu za msingi zinapaswa kushughulikiwa katika jimbo la Arakan ili kutoturudi katika hali ya awali wakati wakimbizi watakapo kuwa wakirejea nchini," amesema mwanadiplomasia huyo, raia wa Denmark ambaye alichukua hatamu ya uongozi wake miezi miwili iliyopita. amemtolea wito kiongozi wa Burma Aung San Suu Kiy "kuvunja vizuizi" kati ya Wabudha na Waislamu.

Kutoroka kwa Rohyngyas, ambao hawajulikani kama wananchi wa Burma, kulisababishwa na operesheni kubwa ya ukandamizaji wa kijeshi ilioanza mwishoni mwa mwezi Agosti baada ya vurugu za kundi linalotaka kujitenga na nchi hiyo. Umoja wa Mataifa na Marekani walilaani operesheni hiyo wakiitaja kama kampeni ya "kufuta kabila".