BURMA-UN-HAKI

Umoja wa Mataifa: Mauaji ya kimbari yaliendeshwa dhidi ya Rohingya Burma

Bangladesh, wakimbizi wa Rohingya wakipewa mablanketi nje ya kambi ya Kutupalong karibu na Cox's Bazar Novemba 24, 2017.
Bangladesh, wakimbizi wa Rohingya wakipewa mablanketi nje ya kambi ya Kutupalong karibu na Cox's Bazar Novemba 24, 2017. REUTERS/Susana Vera

Mauaji ya kimbari yaliendeshwa dhidi ya jamii ya Waislamu wa Rohingya nchini Burma. Kauli hii imetolewa katika kikao maalum cha Tume ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu leo Jumanne (Desemba 5) mjini Geneva.

Matangazo ya kibiashara

Kamishna Mkuu Zeid Ra'ad Al Hussein amelaani mashambulizi yaliyopangwa dhidi ya watu kutoka jamii ya Waislamu wa Rohingya. Takriban watu 626,000 kutoka jamii hiyo tayari wamekimbilia Bangladesh. Na idadi hii inaendelea kuongezeka.

Umoja wa Mataifa tayari umelaani jaribio la kuangamiza jamii ya watu wa Rohingya. Kitendo ambacho kinaendeshwa na viongozi wa nchi hiyo. Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu, Zeid Ra'ad Al Hussein, amekumbusha madhila yaliowakumba Waislamu kutoka jamii hiyo ya watu wachache nchini humo.

"Ukichukulia mashtaka ya hivi karibuni ya mauaji, nyumba kuchomwa huku watu kadhaa wakiwa ndani nyumba hizo, watu kulazimishwa kuyatoroka makazi yao, ukichukulia pia kuwa Rohyingias inatambulika kama jamii au kabila ya watu wachache, kwani wana utamaduni wao, na lugha yao... Kwa vielelezo vyote hivyo, je! kuna mtu yeyote anayeweza kukataa kwamba hatuna hapa mambo yanayoashiria mauaji ya kimbari? Ninaomba Baraza kuchukua hatua zote zinazohitajika ili kukomesha kuanzia sasa hali hii, " Zeid Ra'ad Al Hussein amesema.

Zeid Ra'ad Al Hussein ameomba kuanzishwa kwa utaratibu usio na upendeleo na wa kujitegemea kuchunguza uhalifu uliofanywa nchini Burma. Kwa njia ya moja ambayo tayari inashuhudiwa nchini Syria. Viongozi wa Buram hawataki wachunguzi wa kimataifa katika ardhi yao. Kwa kukabiliana na mashtaka hayo, mwakilishi wa Burma kwenye Tume ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu alipendelea kukosoa tuhuma hizo na kuzitaja kuwa ni hukumu iliyotolewa kimakosa.