KOREA KASKAZINI-UN-MAREKANI-USALAMA

Korea Kaskazini yataja vikwazo vipya dhidi yake ni kama vita

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un ameonya nchi yake kuingiliwa kijeshi.
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un ameonya nchi yake kuingiliwa kijeshi. Reuters/路透社

Korea Kaskazini imesema kuwa vikwazo vilivyochukuliwa hivi karibuni na Umoja wa Mataifa dhidi yake vinaashiria vita dhidi yake. Hayo yanajiri wakati ambapo viongozi wa nchi hiyo wameapa kuendelea na mpango wao wa kutengeneza silaha za nyuklia na majaribio yao ya makombora ya masafa marefu.

Matangazo ya kibiashara

Wakati huo huo kwa mujibu wa shirika la KNCA la Korea Kaskazini, Wizara ya mambo ya nje ya Korea Kaskazini ilisema Korea Kaskazini kuongeza msimamo mkali zaidi ndilo jibu kwa Marekani.

Baraza la ulinzi la Umoja wa Mataifa lilitangaza vikwazo vipya siku ya Ijumaa kufuatia majaribio ya makombora ya masafa marefu ya Korea Kaskazini.

Korea Kaskazini imesema haitishwi na vikwazo hivyo na itaendelea na mpango wake wake wa silaha za nyuklia, hku ikionya nchi yoyote kuingilia kijeshi katika ardhi yake kuwa itakiona chamtima kuni.

Vikwazo hivyo vilipendekezwa na Marekani na kuungwa mkono na wanachama wote 15 wa Baraza la Usalama la Umoja Mataifa. Vikwazo hivyo ni pamoja na kukata mauzo ya mafuta kwa asilimia 90 kwa Korea Kaskazini.

Kwa sasa Korea Kaskazini inakabiliwa na vikwazo vya Umoja wa Mataifa, Marekani na Umoja wa Ulaya.