Pata taarifa kuu
MAREKANI-KOREA KASKAZINI-VIKWAZO-USALAMA

Marekani yawawekea vikwazo maafisa kadhaa wa Korea Kaskazini

Kim Jong-sik na Ri Pyong-chol wamekua wakionekana mara kwa mara wakiwa na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un katika maeneo ya kuyafanyia majaribio ya makombora.
Kim Jong-sik na Ri Pyong-chol wamekua wakionekana mara kwa mara wakiwa na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un katika maeneo ya kuyafanyia majaribio ya makombora. KCNA via REUTERS/File Photo REUTERS
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 2

Mvutano kati ya Marekani na Korea Kaskazini unaendelea, huku Marekani ikichukua hatua ya kuwawekea vikwazo wataalamu wa makombora wa Korea Kaskazini.

Matangazo ya kibiashara

Marekani inasema kuwa maafisa hao wawili wanachangia katika shughuli ya kuundwa kwa makombora ya nchi hiyo.

Hayo yanajiri wakati ambapo Baraza la ulianzi la Umoja wa Mataifa liliiwekea vikwazo vipya Korea Kaskazini siku ya Ijumaa kujibu majaribio yake ya makombora ya masafa marefu.

Kwa mujibu wa wizara ya fedha ya Marekani, Kim Jong-sik na Ri Pyong-chol walikuwa viongozi wakuu katika mpango wa Korea Kaskazini wa makombora ya masafa marefu.

Vikwazo hivyo vipya vya Marekani vitazuia shughuli zozote za maafisa hao wawili zinazofanywa nchini Marekani, na hata kutwaliwa kwa mali yao iliyo nchini Marekani.

Maafisa hao wamekua wakionekana mara kwa mara wakiwa na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un katika maeneo ya kufanyia majaribio ya makombora.

Marekani na Korea Kaskazini wamekua wakitoleana maneno ya kivita, baada ya Korea kaskazini kuendelea na mpango wake wa kutngeneza silaha za nyuklia na kufanya majaribio ya makombora ya masafa marefu, ikiwa ni pamoja na makombora yanayoweza kufika nchini Marekani.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.