Pata taarifa kuu

Kim Jong-un: Marekani isithubutu kuanza vita, itajuta

Kiongozi wa Korea KAskazini Kim Jong-un aionya Marekani.
Kiongozi wa Korea KAskazini Kim Jong-un aionya Marekani. KCNA via REUTERS
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 2

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un ameionya kwa mara nyingne Marekani akisema kuwa ana kibonyezo cha silaha za nyuklia kwenye meza yake wakati wote na kuitaka Marekani kutothubutu kuanza vita.

Matangazo ya kibiashara

Kauli hii alitoa katika hotuba ya mwaka mpya iliyopeperushwa kwa njia ya runinga.

Kim Jong-un alisema Marekani inaweza kuathirika na makombora yake ya masafa marefu.

“Marekani inaweza kufikiwa na silaha za nyuklia za Korea Kaskazini, huo ni kweli na wala sio vitisho, “ amesema kiongozi wa Korea Kaskazini.

Wakati huo huo rais Kim Jong-un alitoa wito kwa Korea Kusini kuja kwenye mazungumzohuku akibaini kwamba Korea Kaskazini itatuma kikosi katika mashindano ya olimpiki ya msmu wa baridi nchini Korea Kusini.

Rais wa Mareani Donald Trump amepuuzia madai hayo ya rais wa Korea Kaskazini akisema kuwa ni upuuzi mtupu.

Vita vya maneneo vimekua vikiendelea kati ya rais Donald Trump na Kim Jong- un, kufuatia majaribio ya makombora ya masafa marefu ya Korea Kasazini pamoja na mpango wake wa silaha za nyuklia

Mwezi Novemba Korea Kaskazini ilifanyia majaribio kombora lake la Hwasong-15 ambalo lilipaa umbali wa kilomita 4,475 mara kumi zaidi kuliko kituo cha safari za anga za juu.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.