Pata taarifa kuu
UFARANSA-CHINA-USHIRIKIANO-UCHUMI

Rais Macron atatamatisha ziara yake China

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, kushoto, akiandamana na Waziri Mkuu wa China Li Keqiang, Januari 9, 2018.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, kushoto, akiandamana na Waziri Mkuu wa China Li Keqiang, Januari 9, 2018. REUTERS/Mark Schiefelbei/Pool

Rais wa China Xi Jinping na mwenzake wa Ufaransa Emmanuel Macron siku ya Jumanne kwa pamoja walishuhudia utiwaji wa saini wa mikataba kadhaa ya kibiashara inayohusisha mabilioni ya dola za Marekani wakati huu Ufaransa ikitaka kuimarisha uhusiano wa kibiashara na China.

Matangazo ya kibiashara

Pande hizo mbili zimetiliana saini mikataba ya nyuklia, anga na kwenye maeneo mengine muhimu wakati wa siku ya pili ya ziara ya rais Emmanuel Macron nchini China.

Hata hivyo Ufaransa imeonya kuhusu kutokuwepo kwa usawa wa kibiashara baina ya mataifa ya Ulaya na China ikisisitiza mikataba hii itumike kumaliza sintofahamu iliyokuwepo.

Rais Macron pia aligusia uhusiano wa nchi za Ulaya, Afrika na China akisema ndio njia pekee ya kukuza uchumi na biashara baina ya mabara haya muhimu duniani.

Rais Macron anatarajiwa kuhitimisha ziara yake nchini China hivi leo na kurejea Ufaransa.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.