Pata taarifa kuu
MAREKANI-KOREA KASKAZINI-USALAMA

Marekani na washirika wake wakubaliana kuchukua hatua dhidi ya Korea Kaskazini

Korea kaskazini imeendelea kukosolewa duniani kwa majaribio yake ya makombora ya masafa marefu na mpango wake w kutengeneza silaha za nyuklia.
Korea kaskazini imeendelea kukosolewa duniani kwa majaribio yake ya makombora ya masafa marefu na mpango wake w kutengeneza silaha za nyuklia. REUTERS/Damir Sagolj
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 1

Marekani na washirika wake wanasema kwa pamoja watachukua hatua kuzuia Korea Kaskazini kuendelea kutengeza silaha za nyuklia lakini pia kuzuia usafirashaji haramu baharini.

Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Mambo wa nje wa Marekani Rex Tillerson na wenzake wa Canada Chrystia Freeland wamekutana jijini Vancouver na kuwaomba viongozi wengine wa dunia kuunga mkono juhudi zao.

Mkutano huo pia umewakutanisha Mawaziri kutoka Korea Kusini na Japan na kwa mara nyingine kuja na msimamo mmoja wa kuzuia Korea Kaskazini kuendelea na mradi wake wa nyuklia.

Mataifa hayo yamekubaliana kuzuia kwa pamoja usafirishwaji wa vifaa vinavyosaidia Korea Kaskazini kuendelea na mradi wake wa nyuklia wanaosema ni hatari kwa usalama wa dunia.

China na Urusi hawakualikwa katika mkutano huo kutokana na msimamo wao wa kuiunga mkono Korea Kaskazini.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.