MAREKANI-URUSI-VIKWAZO-ULINZI

Marekani kutoweka vikwazo vipya dhidi ya Urusi

Rais wa Marekani Donald Trump na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin, mjini Hamburg, Julai 7, 2017.
Rais wa Marekani Donald Trump na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin, mjini Hamburg, Julai 7, 2017. REUTERS/Carlos Barria

Marekani haina mpango wa kuweka vikwazo vipya dhidi ya Urusi licha ya sheria mpya iliyopitishwa mwezi Agosti mwaka jana kuadhibu nchi hiyo kuingilia uchaguzi wa urais wa Marekani wa mwaka 2016, Ikulu ya White House imetangaza.

Matangazo ya kibiashara

White House imebaini kwamba hatua zinazotumika kwa sasa dhidi y Urusi zinatosha.

"Leo tumelieleze bunge la Congress kwamba sheria hii na utekelezaji wake unaathiri mauzo ya kampuni ya Urusi inayotengeneza vifaa vya jeshi," amesema Heather Nauert, msemaji wa wizara ya mshauriano ya kigeni ya Marekani, katika taarifa hiyo.

"Tangu kuanza kutumika kwa sheria hii, serikali za kigeni kwa muono wetu zilijiondoa katika mipango ya kununua silaha na vifaa vingine vya kijeshi ambavyo vingeliingiza mabilioni ya dola katika sekta ya ulinzi ya Urusi."

"Kutokanana maoni haya, tangu sheria ianze kutumika, vikwazo vinavyolenga makampuni au watu binafsi havitakua na umuhimu kwa kuwa sheria inayotumika inatosha kwa kuishawishi Urusi."

Bunge lilipitisha sheria hiyo mwaka jana kwa karibu kauli moja, licha ya upinzani kutoka kwa Donald Trump, ambaye alikua mpango wa kuboresha uhusiano na Urusi. Rais wa Marekani baadae aliipitisha, bila kuokosoa.

Chini ya sheria hii, utawala wa Donald Trump ulikua na muda hadi Jumatatu kuweka vikwazo dhidi ya mtu yeyote atakayehitimisha mikataba mikubwa na sekta ya ulinzi pamoja na idara ya ujasusi ya Urusi , ambayo inakabiliwa na vikwazo kwa kuhusika kwake wakati wa uchaguzi wa urais wa Marekani wa mwaka 2016.