HONG KONG-MAREKANI-USALAMA

Bomu la pili lililotumiwa katika Vita vya Dunia lagunduliwa Hong Kong

Mmoja wa maafisa wa idara ya kutegua mabomu akitazama bomu la Marekani lenye uzito wa kilogramu 450 la vita vya dunia, Hong Kong, Februari 1, 2018.
Mmoja wa maafisa wa idara ya kutegua mabomu akitazama bomu la Marekani lenye uzito wa kilogramu 450 la vita vya dunia, Hong Kong, Februari 1, 2018. AFP

Maafisa wa idara ya kutegua mabomu wamelipua mapema leo alhamisi bomu la Marekani lenye uzito wa kilogramu 450 la tangu Vita vya Dunia.

Matangazo ya kibiashara

Bomu hilo liligunduliwa katika eneo la ujenzi katika eneo la kibiashara linalotembelewa na watu wengi, katikati ya Hong Kong.

Hili ni bomu la pili kugunduliwa kwa muda wa juma moja katika eneo hilo kubwa la ujenziI reli mpya kando na bahari ya eneo la Wanchai.

Baada ya bomu moja kugunduliwa na mfanyakazi siku ya Jumatano asubuhi, polisi walizingira sehemu ndogo ya eneo hilo, huku watu 4,000 wakihamishwa na usafiri kwa kutumia chombo cha Majini kutoka Victoria kwenda Kowloon ulisimama.

"Shughuli zangu za kutegua mabomu zinaweza kuwa mbaya, ngumu na hatari, Lakini sasa hoja zote tatu ziko sahihi," amesema Alick McWhirter, kiongozi wa kikosi cha Idara ya kutegua mabomu.