KOREA KASKAZINI-UN

Watalaam wa UN wasema Korea Kaskazini imeendelea kufanya biashara licha kuwekewa vikwazo

Kiongozi wa Korea Kaskazini  Kim Jong-un
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un KCNA/via REUTERS

Ripoti ya wataalam wa Umoja wa Mataifa inaonesha kuwa Korea Kaskazini ilipata takriban Dola milioni mia mbili mwaka uliopita kutokana na uuzaji wa bidhaa zilizopigwa marufuku katika mataifa ya nje, licha ya kuwekewa vikwazo na Jumuiya ya Kimataifa.

Matangazo ya kibiashara

Watalaam hao wamebaini kuwa, Korea Kaskazini iliuza bidhaa zake katika nchi za China, Urusi na Malaysia ambazo zilishindwa kutii vikwazo vya Jumuiya ya Kimataifa kutoshirikiana na Pyongyang.

Biashara hiyo, imebainika kuwa kuwa ilifanyika kati ya mwezi Januari na Septemba mwaka 2017 licha ya vikwazo vilivyowekwa na Marekan, Umoja wa Mataufa na Umoja wa Ulaya kutokana na mradi wake wa nyuklia.

Mbali na hilo, watalaam hao wamebaini kuwa kumekuwa na ushirikiano wa karibu wa kijeshi kati ya Korea Kaskazini, Syria na Myanmar.