CHINA-MAREKANI-USALAMA

Marekani yashtumiwa na China kwa sera yake ya nyuklia

Maafisa wa jeshi la Marekani wanachunguza bomu la B-53 katika kiwanda cha Pantex, bomu ambalo linapatikana pekee ambapo silaha za nyuklia zinaendelea kutengenezwa, kuhifadhiwa na kudhibitiwa, Amarillo, Texas.
Maafisa wa jeshi la Marekani wanachunguza bomu la B-53 katika kiwanda cha Pantex, bomu ambalo linapatikana pekee ambapo silaha za nyuklia zinaendelea kutengenezwa, kuhifadhiwa na kudhibitiwa, Amarillo, Texas. REUTERS/Photo Courtesy B&W Pantex/Handout

China imeishtumu Marekani kuhusu sera yale ya nyuklia huku ikiomba iachane na mpango huo. Tangazo hilo la China linakuja baada ya Marekani kusema inapanga kupanua mpango wake wa kutengeneza silaha za nyuklia kwa kuunda mabomu madogo.

Matangazo ya kibiashara

Nyaraka iliyotolewa na wizara ya ulinzi ya Marekani siku ya Ijumaa inayojulikana kama Nuclear Posture Review (NPR), inadai kuwa kutengeneza silaha ndogo za nyuklia itasaidia kupambana na fikra kuwa Marekani sio tishio. Silaha hizo ndogo hazina nguvu sana lakini bado zinaweza kusababisha madhara makubwa.

China imesema inapinga "vikali" ukarabati huo wa sera ya Marekani ya nyuklia.

China imesema fikra ya Marekani ya 'Vita vya baridi' haitazaa chochote, bali itakuza tu uadui na nchi nyingi duniani.

Jana Jumapili Waziri wa Ulinzi wa China alisema nchi kama Marekani inayomiliki silaha kubwa za nyuklia duniani, inapaswa kuwa mfano na kuepuka na hatari yoyote kuliko kwenda kinyume.

Hata hivyo Urusi imelaani mpango huo ikisema kuwa haufai.

Sababu kubwa ya kuidhinishwa mpango mpya wa ulizni wa Marekani mwezi jana, ni kukabiliana na "tishio linaloongezeka la mataifa yenye yenye nguvu", kama Uchina na Urusi.

Hivi karibuni Marekani imeitaja Uchina, Urusi Korea kaskazini na Iran kama mataifa yanayoweza kuwa tishio kwake. Na hivyo kuwa na wasiwasi na nchi hizo. Tayari Marekani imeona kuwa silaha zake za nyuklia si tishio tena kwa nchi hizo.