MAREKANI-KOREA KASKAZINI-USALAMA

Michezo ya Olimpiki 2018: Marekani kukutana na Korea Kaskazini

Makamu wa Rais wa Marekani Mike Pence au maafisa wengine kutoka Marekani wanaweza kukutana kwa mazungumzo na viongozi wa Korea Kaskazini wakati wa mashindano ya Michezo ya Olimpiki itakayopigwa Korea Kusini, Waziri Rex Tillerson alisema siku ya Jumatatu.

Waziri wa Mashauriano wa Kigeni wa Marekani Rex Tillerson, Februari 5, 2018 Lima, Peru.
Waziri wa Mashauriano wa Kigeni wa Marekani Rex Tillerson, Februari 5, 2018 Lima, Peru. AFP
Matangazo ya kibiashara

Hivi karibuni Marekani ilitangaza kwamba itajitahidi isiwasiliane na Korea Kaskazini katika mashindano ya Michezo ya Olimpiki nchini Korea Kusini, lakini utawala wa Trump umesema uko tayari kwa mazungumzo na Kim kiongozi wa Korea Kaskazini Jong-Un ili kumshawishi aachane na mpango wake wa nyuklia.

Akiohojiwa nchini Peru wakati wa ziara yake katika Amerika ya Kusini juu ya uwezekano wa mkutano kati ya Mike Pence na ujumbe wa Korea Kaskazini, Waziri wa Mashauriano ya Kigeni wa Marekani, Rex Tillerson, hakupinga uwezekano huo.

"Kuhusu ziara ya Makamu wa Rais nchini Korea Kusini kuhudhuria mashindano ya Michezo ya Olimpiki na ikiwa katakua na fursa ua la ya kukutana na ujumbe wa Korea Kaskazini, nadhani tutaona kitakachotokea," Bw Tillerson aliwaambia waandishi wa habari.

Akihojiwa ili kujua kama alikana mkutano huo, Rex Tillerson alijibu, "Tutaona, tutaona kitakachotokea."

Mike Pence anazuru Alaska, Tokyo, na Seoul kabla ya kuhudhuria sherehe ya ufunguzi wa mashindano ya Michezo ya Olimpiki katika mji wa Pyeongchang siku ya Ijumaa.

Mnamo mwaka 2017, kwa jitihada za Marekani, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liliweka vikwazo vya kiucgumi vya aina tatu dhidi ya Korea Kaskazini, vikwazo ambavyo vinaathiri hasa mauazo yake ya nje ya makaa, uvuvi na sekta ya viwanda. Vikwazo hivi vilichukuliwa baada ya Korea kaskazini kufanya majaribio yake ya makombora, ambayo Marekani na Umoja wa Mataifa walishtumu kwamba yanatishia usalama wa kimataifa.