UTURUKI-EU-USALAMA-HAKI

Bunge la Ulaya lashtumu kuvunjwa kwa haki za binadamu Uturuki

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan.
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan. Yasin Bulbul/Presidential Palace/Handout via REUTERS

Bunge la Ulaya, katika azimio lililopitishwa leo Alhamisi mjini Strasbourg, linasema lina wasiwasi na kuvunjwa kwa uhuru wa msingi nchini Uturuki tangu jaribio la mapinduzi mwezi Julai 2016.

Matangazo ya kibiashara

Bunge la Ulaya limeomba kuachiliwa kwa maelfu ya watu waliofungwa kwa makosa ya kutoa maoni yao.

Hata hivyo, Bunge la Ulaya halikutoa msimamo wowote taarifa yake kuhusu hatua ya Uturuki kuingilia kijeshi katika neo la Wakurdi la Afrin, kaskazini magharibi mwa Syria.

Bunge la Ulaya "limeelezea wasiwasi wake" kuhusu kuvunjwa kwa haki za msingi, uhuru na utawala wa sheria nchini Uturuki, na pia ukosefu wa uhuru kwa mahakama.

Bunge hilo limelaani kukamatwa bila hatia yoyote na kufungwa kwa maelfu ya watu ".

Bunge la Ulaya "limeshauri mamlaka ya Uturuki kufungua mara moja na bila masharti watu wote waliofungwa wakati walipokua wakishughuli yao halali na kutumia uhuru wao wa kujieleza na kushirika katika mashirika na ambao walifungwa bila ushahidi wpowote kuthibitisha kuwa ni makosa ya jinai ".

Azimio hilo, lililoungwa mkono na makundi yote ya kisiasa, linashtumu kufungwa kwa wabunge, waandishi wa habari, wanafunzi na wananchi wa kawaida chini ya "sheria dhidi ya Ugaidi".

Siku y Jumatatu Uturuki ilitangaza kuwa ilikawamata watu 573 ambao walikosoa kuingilia kwake kijeshi nchini Syria.