URUSI-AJALI

Urusi yachunguza sababu ya ajali ya Antonov iliyoua watu 71

Ndege aina ya Antonov An-148 ya shirika la ndege la Saratov Airlines, ilianguka karibu na mji wa Moscow muda mfupi baada ya kuondoka kwenye uwanja wa ndege wa Domodedovo ( kwenye picha).
Ndege aina ya Antonov An-148 ya shirika la ndege la Saratov Airlines, ilianguka karibu na mji wa Moscow muda mfupi baada ya kuondoka kwenye uwanja wa ndege wa Domodedovo ( kwenye picha). www.domodedovo.ru

Wachunguzi wa Urusi wanachunguza sababu ya ajali ya ndege aina ya Antonov iliyoanguka karibu na Moscow na kuua watu 71 siku ya Jumapili.

Matangazo ya kibiashara

Maafisa hao wa Urusi watachunguza mambo yote ambayo yanaweza kuwa ni sababu ya ajali hiyo ikiwani pamoja na masuala ya hali ya hewa, sababu ya kibinadamu au tatizo la kiufundi - lakini bila kufutilia mbali suala la ugaidi.

Ndege hiyo aina ya Antonov An-148 ya shirika la ndege la Saratov Airlines, ilianguka karibu na mji wa Moscow siku ya Jumapili muda mfupi baada ya kuondoka kwenye uwanja wa ndege wa Domodedovo.

Ndege ilipoteza mawasiliano na mitambo ya uwanja wa ndege, dakika nne baada ya kuondoka kuelekea Orsk, mji wa Urals. Ilianguka katika wilaya ya Ramenski, kilomita 70 kusini mashariki mwa Moscow, karibu na kijiji cha Stepanovskoye.

"Abiria 65 na wafanyakazi sita waliokua katika ndege hiyo, wote walipoteza maisha," ofisi maalumu ya mashita katika masuala ya usafiri ilitangaza katika taarifa yake.

Uchunguzi umefunguliwa rasmi ili kujua uwezekano wa ukiukwaji wa sheria za usalama, Kamati ya Uchunguzi ya Urusi imetangaza. "

Vladimir Putin ametoa rambi rambi zake kwa familia na kufuta ziara yake iliyokua imepangwa leo Jumatatu katika mji wa Sochi, kusini mwa Urusi