KOREA KASKAZINI-KOREA KUSINI-USHIRIKIANO

Kim Jong-un: Naishukuru Korea Kusini kwa makaribisho mema

RAis wa Korea Kusini Moon Jae-in akimsabahi Kim Yo-jong, dada wa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un.
RAis wa Korea Kusini Moon Jae-in akimsabahi Kim Yo-jong, dada wa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un. KCNA/via REUTERS

Siku nne baada ya kuzinduliwa kwa mashindano ya olimpiki katika kijiji cha Pyeongchang kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un ameishukuru Korea Kusini kwa kuukaribisha ujumbe kutoka Kaskazini uliohudhuria mashindano hayo ya msimu wa baridi.

Matangazo ya kibiashara

Kuhudhhuria kwa Korea Kaskazini kumekuwa kwa mchango mkubwa kwa uhusiano kati ya nchi hizo, ambazo uhusiano wao ulidorora kwa miaka kadhaa.

Ujumbe wa Korea Kaskazini katika mashindano ya olimpiki uliongozwa na dada yake rais, Kim Yo-jong na tayari umerejea nyumbani kutoka Pyeongchang.

Bi Kim na mkuu wa nchi asiye na madaraka Kim Yong-nam waliakuwa miongoni mwa maafisa wakuu waliokuwa kwenye ujumbe wa Korea Kaskazini kuzuru Korea Kusini tangu vita vya Korea Kaskazini miaka ya 1950.

Kwa mujibu wa shirika la habari la serikali la KCNA, Kim Jong-un aliishukuru Korea Kusini kwa kuupigia debe uwepo wake katika mashindano hayo.