URUSI-MAREKANI-UCHAGUZI-USALAMA

Urusi yafutilia mbali shutma za kuingilia uchaguzi wa Marekani

Rais wa Urusi Vladimir Putin na msemaji wake Dmitry Peskov, Sochi, kusini mwa Urusi, Oktoba 11, 2017.
Rais wa Urusi Vladimir Putin na msemaji wake Dmitry Peskov, Sochi, kusini mwa Urusi, Oktoba 11, 2017. AFP

Ikulu ya Kremlin leo Jumatatu imefutilia mbali madai ya kuingilia uchaguzi wa urais wa Marekani. Kauli hii ya Urusi inakuja siku chache tu baada ya raia 13 wa Urusi kupatikana na hatia ya kuhusika kuingilia uchaguzi.

Matangazo ya kibiashara

Uchaguzi ambao Donald Trump alibuka mshindi dhidi ya mshindani wake Hillary Clinton aliyepeperusha bendera ya chama cha Democratic.

Mahakama ya Marekani imetoa mwelekeo mpya wa uchunguzi na mwendesha mashtaka maalum Robert Mueller, akiwaweka hatiani watu13 ikiwa ni pamoja na mfanyabiashara maarufu, mshirika wa karibu wa Vladimir Putin.

Lakini kwa upande wa ikulu ya Kremlin, ambayo imendelea kufutilia mbali madai hayo ya kungilia uchaguzi wa Marekani kwa kumpatishia ushindi Donald Trump, inasema ni viongozi tu wa kawaida ambao wanaonekana kushtumiwa na sio Urusi.

"Hatuoni ushahidi wowote wa mtu yeyote kuingilia katika uchaguzi wa urais wa Marekani," msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov amewaambia waandishi wa habari.

Watuhumiwa wote (13 raia wa Urusi na makampuni matatu) wanashutumiwa kula njama ya kudanganya Marekani, watatu miongoni mwao pia wanashutumiwa na kughushi hati za benki na wengine watano wanashutumiwa wizi sugu wa kitambulisho.

Evgeny Prigojine, mshirika wa karibu wa Rais Vladimir Putin ni miongoni mwa washutumiwa hawa. Kwa mujibu wa hati ya mashtaka ya Marekani, Bw Prigojine anadaiwa kuwa alifadhilikundi hili kwa lengo la "kuchochea vurugu katika mfumo wa kisiasa wa Marekani".

Hati ya mashtaka, hata hivyo, haionyeshi uhusiano wowote kati ya timu ya kampeni ya Donald Trump na serikali ya Urusi.

Hakuna "dalili kwamba serikali ya Urusi inahusishwa" wakati ambapo hati ya mashitaka ya Marekani inabaini tu "wananchi wa Urusi," Peskov ameendelea.

"Ndiyo sababu tunsema tukisisitiza kwamba tutaendelea kuchukulia ushahidi huo kama usio na msingi," ameongeza.