UTURUKI-USALAMA-HAKI

Uturuki yatoa waranti dhidi ya askari 17

Watu wanaoshtumiwa kuwa na uhusiano na Fethullah Gulen waendelea kukamatwa Uturuki.
Watu wanaoshtumiwa kuwa na uhusiano na Fethullah Gulen waendelea kukamatwa Uturuki.

Mamlaka ya Kituruki imetoa waranti mpya za kukamatwa kwa askari 170 wanaoshutumiwa kuwa na uhusiano na kundi la Fethullah Gulen, ambaye anashutumiwa kupanga jaribio la mapinduzi lililotibuliwa mwezi Julai 2016, kwa mujibu wa shirika la habari la Anatolia.

Matangazo ya kibiashara

Miongoni mwa watu wanaolengwa na operesheni hii ni askari waliostaafu, wengine ambao tayari wamefutwa kazi au ambao bado wanahudumu katika jeshi. Askari ishirini na mbili walikamatwa siku ya Jumatatu, shirika la habari la serikali Anatolia limearifu.

Watu hawa walikuwa na mawasiliano ya simu na wanachama maarufu wa kundi hilo linaloongozwa na Fetthulah Gulen, shirika la habari la Anatolia limeongeza.

Fethullah Gülen, ambaye anaeishi uhamishoni nchini Marekani tangu mwaka 1999, amekua akiombwa na serikali ya Uturuki kusafirishwanchini humo.

Bw Gulen amekanusha madai yoyote ya kushiki katika jaribio la mapinduzi la mwezi Julai 2016 ambalo liligharimu maisha ya watu 250 na kusababisah maafisa kadhaa wa serikali kukamatwa.