MAREKANI-MONTENEGRO-USALAMA

Ubalozi wa Marekani washambuliwa kwa gruneti Podgorica, Montenegro

Podgorica, mji mkuu wa uchumi wa Montenegro, ambapo ubalozi wa Marekani umeshambuliwa kwa gruneti.
Podgorica, mji mkuu wa uchumi wa Montenegro, ambapo ubalozi wa Marekani umeshambuliwa kwa gruneti. Milos58/CC/Wikimedia Commons

Mtu mmoja amejilipua mbele ya ubalozi wa Marekani huko Podgoric, nchini Montenegro baada ya kurusha gruneti ndani ya jengo la ubalozi huo usiku wa Jumatano kuamkia leo Alhamisi, serikali ya Montenegro imetangaza.

Matangazo ya kibiashara

"Katikati ya usiku wa manane, mbele ya jengo la ubalozi wa Marekani, Montenegro, mtu asiyejulikana amejilipua na kifaa cha kulipuka, kabla ya kurusha kifaa kinachofananishwa na gruneti (...) ndani ya jengo la ubalozi ", kwa mujibu wa serikali ya Montenegro.

"Kuna uwezekano kuwa kifaa hiki kilikua ni gruneti iliyorushwa kwa mmono. Polisi inaendelea na uchunguzi, chini ya uongozi wa mwendesha mashitaka na polisi ya Montenegro," kwa mujibu wa serikali iliyoandika kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Montenegro ilijiunga na Jumuiya ya Kujihami ya Nchi a Magharibi (NATO) mnamo mwezi Mei 2017, hali ambayo inazua mvutano na upinzani kutoka sehemu kubwa ya wakazi wa nchi hii ndogo yenye wakazi 660,000. Tangazo la kujiunga kwa taifa hili lilisababisha maandamano makubwa mwaka 2015.

Itafahamika kwamba ubalozi wa Marekani huko Sarajevo ulilengwa na shambulizi la kigaidi mnamo Oktoba 2011.