MAREKANI-KOREA KASKAZINI-VIKWAZO-USALAMA

Marekani kuweka vikwazo vipya dhidi ya Korea Kaskazini

Utawala wa Marekani unasema "utaendelea na msimamo wake thabiti kama Korea Kaskazini itakua bado haijasitisha vitisho kwa marekani na washirika wake.
Utawala wa Marekani unasema "utaendelea na msimamo wake thabiti kama Korea Kaskazini itakua bado haijasitisha vitisho kwa marekani na washirika wake. REUTERS/Toru Hanai

Utawala wa Donald Trump umepanga kutangaza leo Ijumaa vikwazo vipya dhidi ya Korea ya Kaskazini, kwa mujibu wa afisa mmoja wa ngazi ya juu nchini Marekani.

Matangazo ya kibiashara

Vikwazo hivi vikubwa ambavyo vilikua bado havijachukuliwa mpaka sasa vitailazimu Pyongyang kusitisha mipango yake ya nyuklia na majaribio ya makombora ya masafa marefu.

Trump anatarajiwa kutangaza vikwazo vipya leo Ijumaa asubuhi wakati wa hotuba yake katika mkutano mkuu wa kila mwaka wa Conservative Political Action Conference (CPAC), kabla wizara ya fedha kutoa maelezo baadaye mchana.

Hivi ni vikwazo vipya vikubwa zaidi dhidi ya serikali ya Korea Kaskazini," afisa wa ngazi ya juu katika utawala wa Trump, ambaye hakutaka kutaja jina, ameliambia shirika la habari la Reuters.

Makamu wa Rais Mike Pence alitangaza wakati wa ziara yake mjini Tokyo wiki mbili zilizopita, kabla ya kuhudhuria sherehe ya ufunguzi wa mashindano ya Olimpiki huko Pyeongchang (Korea Kusini), kwamba vikwazo vikali vitachukuliwa hivi karibuni dhidi ya Korea Kaskazini, "utawala wa kidhalimu na uchokozi duniani".

Katika mkutano wa CPAC jana Alhamisi, Pence alisema kuwa Marekani "itaendelea na msimamo wake thabiti kama Korea Kaskazini itakua bado haijasitisha vitisho kwa nchi yetu na washirika wetu, au hadi pale itaachana mara moja na mipango yake ya nyuklia na majaribio ya makombora ya masafa marefu ".

Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Nikki Haley, alisema jana Alhamisi katika hotuba yake katika Chuo Kikuu cha Chicago kuwa vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini vina athari kwani nchi hii sasa ina kiwango kidogo cha fedha kwa kufanya majaribio ya makombora ya masafa marefu.

"Sababu hii ndio ilipelekea utawala wa Kim (Jong-un) kufufua mawasiliano na Korea Kusini na kufanya operesheni ya mawasiliano katika mashindano ya Olimpiki." Kutuma wanamichezo wa pom-pom katika mji wa Pyeongchang (korea Kusini) ilikuwa ishara ya ukosefu, " amesema balozi Nikki Haley.