IRAN-MAREKANI-USHIRIKIANO

Marekani kuchukua vikwazo dhidi ya Iran

Nikki Haley (picha), balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa, hakuwaambia waandishi wa habari hatua ambazo zinaweza kuchukuliwa dhidi ya Iran.
Nikki Haley (picha), balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa, hakuwaambia waandishi wa habari hatua ambazo zinaweza kuchukuliwa dhidi ya Iran. REUTERS/Eduardo Munoz

Marekani imetishia kuweka vikwazo dhidi ya Iran, baada ya Urusi kutumia kura yake ya turufu kupinga azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linaloishtumu Iran kuhusika na kuwapa silaha waasi wa Houthi katika vita nchini Yemen.

Matangazo ya kibiashara

"Ikiwa Urusi itaendelea kuunga mkono vitendo vya Iran, Marekani na washirika wake watalazimika kuchukua vikwazo," alisema Nikki Haley, balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa alipokua njiani akielekea Honduras.

Nikki Haley hakuwaambia waandishi wa habari hatua ambazo zinaweza kuchukuliwa.

Urusi ilitumia kura yake ya turufu kupinga azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa jana Jumatatu. Baraza la Usalma la Umoja wa Mataifa lilielezea wasiwasi wake baada ya wachunguzi wa Umoja wa Mataifa kupata ushahidi kwamba Iran haikuweza kuheshimu vikwazo vilivyowekwa na Umoja wa Mataifa kuhusu silaha kwa waasi waKishia wa Houthi.

Uamuzi wa rasimu uliwasilishwa na Uingereza, kwa ushirikiano na Marekani na Ufaransa.

Kira hii ya turufu ya Urusi ni pigo kwa Marekani, ambayo imekuwa ikiomba kwa miezi kadhaa ili Iran ichukuliwe vikwazo na Umoja wa Mataifa. Pia Marekani inataka kurekebisha "makosa mabaya" ya mpango wa nyuklia wa Iran.

Donald Trump alikubali mnamo Januari 12, kwa "mara ya mwisho", kuongeza muda kwa mikataba ya kiuchumi dhidi ya Iran iliyofutwa chini ya makubaliano ya 2015 kuhusu shughuli za nyuklia za Jamhuri ya Kiislamu (Iran).