Pyongyang kujadili na Marekani kuhusu silaha za nyukilia

Rais wa China Xi Jinping na mwenzake wa Korea Kaskazini Kim Jong-un, Machi 28, 2018 Beijing.
Rais wa China Xi Jinping na mwenzake wa Korea Kaskazini Kim Jong-un, Machi 28, 2018 Beijing. CCTV / AFP

Korea Kaskazini imeiambia Marekani kwa mara ya kwanza kuwa iko tayari kujadili kuhusu mpango wa kuondoa silaha za nyuklia katika rasi ya Korea wakati wa mkutano kati ya Donald Trump na Kim Jong-un, kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters likinukuu maafisa wawili waandamizi wa serikali ya Marekani.

Matangazo ya kibiashara

Mawasiliano ya chini kwa chini na ya moja kwa moja yalifanyika hivi karibuni kati ya serikali hizi mbili ambazo wawakilishi wa Korea Kaskazini waliwapeleka ujumbe huo washiriki wao wa Marekani, amesema mmoja wa viongozi hawa ambaye hakutaja jina.

Utawala wa Marekani ulitegemea uhakikisho kutoka Korea Kusini, ambayo ilifanya kazi kama mpatanishi kati ya Pyongyang na Washington.

"Marekani ina uthibitisho kwamba Kim Jong-un yuko tayari kujadili kuhusu mpango wa kuondoa silaha za nyuklia katika rasi ya Korea," amesema afisa mwengine wa serikali ya Trump.

Kwa upande mwingine, Korea Kaskazini ina wasiwasi kuhusu "mpango wa kuondoa silaha za nyuklia katika rasi ya Korea", ambapo Marekani inafafanua kama kuachana na mpango wa kijeshi wa nyuklia wa Korea Kaskazini.

Hivi karibuni Korea Kaskazini ilisema itafikiria uwezekano wa kuachana na silaha zake za nyuklia ikiwa Washington itaondoa askari wake kutoka Korea Kusini - ambako askari 28.500 wa Marekani wanapiga kambi.

Mkutano wa kihistoria na usio wa kawaida unaoandaliwa kati ya rais wa Marekani na kiongozi wa Korea Kaskazini, kupitia jitihada za Kim na ambapo Trump anasema anasubiri kwa hamu ", umepangwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Mei.