IRAN-MAREKANI-USHIRIKIANO

Rouhani: Marekani "itajuta" ikiwa itakiuka makubaliano ya nyuklia ya Iran

Rais wa Iran Hassan Rouhani ameonya leo Jumatatu kuwa Marekani "itajuta" ikiwa itajitoa kwenye mpango wa nyuklia wa Iran "kama anavyotishia kufanya Rais Donald Trump".

Picha iliyotolewa na Ofisi ya Hassan Rouhani Inaonyesha Rais wa Iran katika Sherehe huko Tehran ya Siku ya Kitaifa ya Teknolojia ya nyuklia, Aprili 9, 2018.
Picha iliyotolewa na Ofisi ya Hassan Rouhani Inaonyesha Rais wa Iran katika Sherehe huko Tehran ya Siku ya Kitaifa ya Teknolojia ya nyuklia, Aprili 9, 2018. AFP
Matangazo ya kibiashara

"Hatutakuwa wa kwanza kukiuka makubaliano lakini Marekani inapaswa kufahamu kuwa itajuta ikiwa itakiuka makubaliano hayo," amesema Bw Rouhani katika hotuba ya kushehereka Siku ya Kitaifa ya Teknolojia ya Nyuklia.

"Tmejiandaa zaidi kuliko wanavyofikiri, na wataona kwamba ikiwa watakiuka mkataba huu, kwa wiki moja, chini ya wiki moja, wataona matokeo," Bw Rouhani ameongeza.

Ikiwa Marekani "itajitoa (kwenye makubaliano), itakuwa na maana kuwa hawatekelezi maneno yao. Hali hiyo itaharibu sifa zao na heshima yao katika ngazi ya kimataifa," amesema rais wa Iran.

Makubaliano kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran ulihitimishwa mnamo mwezi Julai 2015 kati ya Jamhuri ya Kiislam ya Iran na Kundi la nchi Sita (Ujerumani, China, Marekani, Ufaransa, Uingereza, Urusi na Ujerumani).