URUSI-MAREKANI-VIKWAZO

Urusi kuchukua hatua za kulipiza kisasi baada ya vikwazo vya Marekani

Waziri Mkuu wa Urusi Dmitry Medvedev aionya Marekani kufuatia vikwazo vipya dhidi ya Moscow.
Waziri Mkuu wa Urusi Dmitry Medvedev aionya Marekani kufuatia vikwazo vipya dhidi ya Moscow. Reuters/路透社

Waziri Mkuu wa Urusi Dmitry Medvedev leo Jumatatu ameagiza serikali yake kuandaa orodha ya hatua kali za ulipizaji kisasi kufuatia vikwazo vipya vya Marekani dhidi ya Urusi, Shirika la habari la Interfax limearifu.

Matangazo ya kibiashara

Medvedev amesema vikwazo vya Marekani dhidi ya Urusi havikubaliki na ni si halali, na kuongeza kwamba Urusi inajiandaa kujibu, shirika la habari la Interfax imeongeza.

Ikulu ya Kremlin, hata hivyo, imebaini kwamba uamuzi wowote kutoka kwake kuhusu kulipiza kisasi "utachukua muda".

Waziri Mkuu pia amesema kuwa serikali yake inatarajia kuanzisha mpango wa kusaidia makampuni ya yaliyowekewa vikwazo na Marekani.

Siku ya Ijumaa wizara ya mambo ya nje ya Urusi ilisema kuwa Urusi itajibu kwa hatua kali kwa vikwazo vipya vya marekani.

Wiki iliyopita Marekani iliwawekea vikwazo vipya maafisa 24 wa Urusi, ikiwa ni pamoja na vigogo na viongozi wa serikali walio karibu na rais wa nchi hiyo Vladimir Putin, na makampuni na mashirika 14 kwa "shughuli hasidi" za Moscow zinazolenga kuhatarisha demokrasia ya nchi za Magharibi, Waziri wa Fedha Steve Mnuchin alisema.