KOREA KASKAZINI-MAREKANI-USALAMA

Kim Jong Un atangaza rasmi "mazungumzo" na Marekani

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un amezungumzia hadharani kwa mara ya kwanza katika mkutano wa chama tawala katika mji mkuu wa nchi hiyo, Pyongyang, "mazungumzo" na Marekani, wakati ambapo kunaandaliwa mkutano wa kihistoria kati ya kiongozi huyo na rais wa Marekani Donald Trump.

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un atarajiwa kukutana na rais wa Marekani Donald Trump.
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un atarajiwa kukutana na rais wa Marekani Donald Trump. ©SAUL LOEB, Ed JONES / AFP
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Marekani alikubali mwezi uliopita kukutana na rais wa Korea Kaskazinii, mkutano ambao utakua wa kwanza katika historia kati ya rais wa Marekani madarakani na kiongozi wa Korea Kaskazini.

Katika mkutano wa maafisa waandamizi wa chama cha tawala, Bw Kim walijadili "maendeleo ya sasa kuhusu uhusiano wa Korea mbili na matarajio ya mazungumzo kati ya Marekani na Korea Kaskazini", shirika la habari la Korea Kaskazini la KCNA limearifu.

Kim Jong Un alitoa ripoti "kuhusu hali inayoendelea katika rais ya Korea" na hasa mkutano mwingine, uliopangwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu pamoja na Korea Kusini, kwa mujibu wa shirika la habari la KCNA.

Trump alitangaza mwezi uliopita kuwa alikubali mkutano na rais wa Korea Kaskazini kujadili uwezekano wa kuondoa silaha za nyuklia katika rasi ya Korea. Lakini Pyongyang hakuwahi kuzungumza hadharani juu ya mkutano huo tangu mwaliko wa Kim kupelekwa kwa rais wa Marekani na viongozi wa Korea Kusini.