KOREA KASKAZINI-KOREA KUSINI-USHIRIKIANO

Kim Jong-un na Moon Jae-wataka "utawala wa amani"

Rais wa Korea Kusini Jae-in na mwenzake wa Korea Kaskazini Kim Jong-un wamesema baada ya mkutano wao wa kihistoria Ijumaa wiki hii mjini Panmunjeom, Korea Kusini, kwamba watajikita kwa kutunza amani katika rasi ya Korea.

Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in (kulia) na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un wako tayari kuleta amani katika rasi ya Korea.
Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in (kulia) na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un wako tayari kuleta amani katika rasi ya Korea. Korea Summit Press Pool/Pool via Reuters
Matangazo ya kibiashara

Korea mbili zitatafuta mwaka huu njia ya kukomesha vita visivyorudi, kwa mujibu wa taarifa ya pamoja iliyotolewa leo Ijumaa baada ya mkutano wa kihistoria, miaka 65 baada ya kumalizika kwa uhasama kati ya majeshi badala ya mkataba wa amani.

Majirani hawa wawili watajaribu kukutana na Marekani, labda pia na china - nchi mabazo zilisaini makubaliano ya kusitisha mmapigano, kwa lengo la "kutangaza mwisho wa vita na kuanzisha utawala wa amani wa kudumu na ulio imara", Nakala hiyo imesema.

Wawili hawa wamesema "Korea Kusini na Korea Kaskazini zinathibitisha lengo la pamoja la kupata amani ya kudumu katika rasi ya Korea. "

Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in atazuru Pyongyang mwaka huu, na nchi hizo mbili zitafanya mkutano mwingine wa familia zilizojitenga tangu kumalizika kwa vita, miaka 65 iliyopita.

Rais wa Korea Kusini Jae-in na mwenzake wa Korea Kaskazini Kim Jong-un.
Rais wa Korea Kusini Jae-in na mwenzake wa Korea Kaskazini Kim Jong-un. Korea Summit Press Pool/Pool via Reuters

Kwa upande wake, Kim Jong-un ameahidi kutorejelea "matokeo mabaya yaliyozikumba nchi hizi mbili" na kuhakikisha kuwa mkataba na mwenzake wa Korea Kusini umeanza kutkelezwa, jambo ambalo hakikuwezekana kwenye mikataba iliyotangulia

China na Marekani zimepongeza mkutano kati ya viongozi wa Korea hizo mbili.