Pata taarifa kuu
IRAN-EU-MAREKANI-USALAMA

Trump atengwa, EU yajaribu kuokoa mpango wa nyuklia wa Iran

Mawaziri wa wa mambo ya nje wa Ufaransa, Jean-Yves Le Drian, Ujerumani Sigmar Gabriel, Uingereza Boris Johnson na Mkuu wa sera za mambo ya Nje wa Ulaya Federica Federica Mogherini baada ya mkutano kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran, Brussels, Januari 11, 201
Mawaziri wa wa mambo ya nje wa Ufaransa, Jean-Yves Le Drian, Ujerumani Sigmar Gabriel, Uingereza Boris Johnson na Mkuu wa sera za mambo ya Nje wa Ulaya Federica Federica Mogherini baada ya mkutano kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran, Brussels, Januari 11, 201 REUTERS/Francois Lenoir
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 3

Siku moja baada yakujitoa kwenye mkataba kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran, Donald Trump anajikuta ametengwa na washirika wake wa Ulaya, ambao tangu Jumatano wako katika mbio za kujaribu kuishawishi Iran kutoanzisha tena mpango wake silaha za nyuklia Mashariki ya Kati.

Matangazo ya kibiashara

Rais wa Marekani, ambaye siku ya Jumanne wiki hii alichukua msimamo mkali kwa kurejesha vikwazo vyote vilivyofutwa tangu kusainiwa kwa mkataba huo mnamo mwaka 2015, alielezea tishio lake: kama Iran "itaanzisha mpango wake wa nyuklia", " kutakuwa na madhara makubwa. "

Saudi Arabia, moja ya nchi chache, na Israeli, ziliunga mkono uamuzi wa Washington dhidi ya hasimu wao. Wakati huo huo Iran imetoa onyo lake.

Saudi Arabia imepuuzia onyo hilo na kusuma kuwa itakabiliana na stishio lolote la Iran.

"Ikiwa Iran itaendelea na mpango wake wa nyuklia, tutajitahidi kufanya vivyo hivyo," Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia, Adel al-Jubeir, ameonya kwenye kituo cha habari cha Marekani cha CNN mkuu wa diplomasia ya Ufalme wa Sunni, Adel al-Jubeir.

Hatari za kuongezeka kwa mvutano huo ni hofu ya mgogoro mpya kati ya nchi hizi mbili. Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Jim Mattis, alisema siku ya Jumatano kuwa diplomasia imebakia njia pekee kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Lakini kwa sasa, Umoja wa Ulaya umeanzisha mazungumzo bila Wamarekani, ambapo Uingerez imetaka "kuepuka hatua yoyote ambayo ingezuia pande zingine kuendelea kufanya kazi ili mkataba huo uendelea kutekelezwa".

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, ambaye anaendelea na msimamo wake baada ya kushindwa kufuata msimamo wa Donald Trump, alizungumza kwa simu kwa muda mrefu na mwenzake wa Irani Hassan Rohani.

Kwa mujibu wa serikali ya Ufaransa, wawili hao "wataendelea kazi yao ya pamoja" ili kuendelea kutekeleza "mpango wa utekelezaji" wa mwaka 2015, kupitia "makundi ujumbe" kutoka Iran na Umoja wa Ulaya yatakayowekwa "bila kuchelewa". Hassan Rohani, mmoja wa waansisi wa mkataba huo, amemwambia Emmanuel Macron kwamba atafanya "kilio chini ya uwezo wake ili kusalia kwenye mkataba," ofisi ya rais wa Ufaransa imeeleza.

"Tutaheshimu mkataba na tutafanya tunachokiweza ili kuhakikisha kwamba Iran inaendelea kushikilia majukumu yake," ameongeza Kansela wa Ujerumani Angela Merkel.

Maaziri wa mambo ya nje wa nchi tatu za Ulaya zilizosaini makataba huo (Ufaransa, Ujerumani, Uingereza) watakutana mapema wiki ijayo na mwenzao wa Irani Mohammad Javad Zarif, amesema Waziri wa Ufaransa Jean-Yves Le Drian.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.