MAREKANI-IRAN-NYUKLIA-USALAMA

Washington yatishia kuiwekea Iran "vikwazo vikali vya kihistoria

Marekani imeahidi kuiwekea Iran vikwazo vikali vya kihistoria, ambavyo haijawahi kuiweke nchi yoyote katika historia ya taifa hilo. Marekani imesema vikwazo hivyo vitaipelekea Iran kuzingatia orodha ya masharti makubwa kumi na mbili ya "mkataba mpya" , baada ya Marekani kujitoa kwenye mkataba kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo Washington, Mei 21, 2018.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo Washington, Mei 21, 2018. REUTERS/Jonathan Ernst
Matangazo ya kibiashara

Wakati huo huo Rais wa Iran Hassan Rouhani, amepinga vikali kauli hiyo ya Marekani iliyotolewa na waziri wake wa mambo ya nje Mike Pompeo, ambaye alisema kuwa taifa lake linatarajia kuiwekea Irani vikwazo ambavyo haijawahi kuiwekea taifa lolote katika historia ya taifa hilo.

"Iran haitakuwa tena na kadi nyeupe ili kutawala Mashariki ya Kati," Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo alisema akionyesha "mkakati mpya" baada ya uamuzi tata uliotangazwa Mei 8 na Rais wa Marekani Donald Trump.

"Wewe ni nani kuchukua uamuzi dhidi ya Iran na dunia?" Wakati wa maazimio hayo umekwisha, "amejibu Rais wa Iran Hassan Rohani.

Pompeo ametaja mambo kumi na mbili ambayo Washington inautaka utawala wa Tehran kufanya,ikiwa ni pamoja na suala la Iran kuondoa vikosi vyake, Syria na kusitisha misaada kwa waasi wa Yemen. Amesisitiza kwa mataifa yanapaswa kuunga mkono hatua hizo za Marekani.

Kwa mikakati iliyowekwa hii leo,tunahitaji uungwaji mkono na washirika wetu ndani ya ukanda wetu na marafiki zetu wa Ulaya pia kutuunga mkono kukabiliana na Iran.

Ametishia pia kwamba mataifa yatakayokiuka masharti ya vikwazo dhidi ya Iran,kwamba yatakumbana na hali ngumu.

Uamuzi wa Marekani wa kujitoa kwenye mktaba uliofikiwa mnamo mwaka 2015 na mataifa yenye nguvu (Marekani, Urusi, China, Ufaransa, Uingereza na Ujerumani) na serikali ya Tehran ili kuizuia kupata bomu ya atomiki ulighadhabisha nchi za Ulaya, waliokuwa wamejaribu, bila mafanikio, kuzungumza na Washington kuhusu ufumbuzi wa "kuufanya mgumu" na kukosoa tabia nyingine za Iran zinazoonekana "kuhatarisha" usalama katika ukanda huo.