Pata taarifa kuu
IRAN-EU-MAREKANI-USALAMA

Iran yatoa masharti kusalia kwenye mkataba wa nyuklia

Kiongozi wa juu wa Iran Ayatolah Ali Khamenei pia amefutilia mbali masharti yaliyotakiwa na Marekani kurudi kwenye mkataba kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran.
Kiongozi wa juu wa Iran Ayatolah Ali Khamenei pia amefutilia mbali masharti yaliyotakiwa na Marekani kurudi kwenye mkataba kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran. ir/Handout via REUTERS
Ujumbe kutoka: RFI
1 Dakika

Kiongozi wa juu nchini Iran Ayatolah Ali Khamenei ametangaza masharti kadhaa kwa nchi yake kusalia kwenye mkataba wa nyuklia wa Iran na mataifa yenye nguvu duniani.

Matangazo ya kibiashara

Miongoni mwa masharti ambayo kiongozi huyo ameyatangaza kwa nchi za magharibi ikiwa wanataka nchi yake isalie kwenye mkataba huo ni pamoja na kulinda biashara ya mafuta ya Iran pamoja na biashara nyingine.

Chini ya makubaliano ya sasa ambayo nchi ya Marekani imejitoa, Iran ilikubali kusitisha shughuli zake za urutubishaji wa nyuklia na kuondolewa vikwazo na mataifa ya magharibi.

Nchi za Uingereza, Ufaransa na Ujerumani hata hivyo zimekuwa mstari wa mbele kujaribu kunusuru mktaba huo huku Iran ikisema itaanza upya mpango wake wa nyuklia labda tu mashrati yake yatekelezwe.

Khamenei pia amesema nchi yake haitajihusisha kamwe katika mazungumzo yoyote na Marekani ikidai taifa hilo limesaliti dunia na hawawezi kuliamini tena.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.