MAREKANI-KOREA KASKAZINI-USALAMA

Marekani na Korea Kaskazini zaendelea na maandalizi ya mkutano

Mjumbe wa Korea Kaskazini Kim Yong-chol amewasili New York kwa maandalizi ya mkutano kati ya rais wa Marekani Donald Trump na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un, Mei 30, 2018.
Mjumbe wa Korea Kaskazini Kim Yong-chol amewasili New York kwa maandalizi ya mkutano kati ya rais wa Marekani Donald Trump na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un, Mei 30, 2018. REUTERS/Lucas Jackson TPX IMAGES OF THE DAY

Waziri wa Mashauriano ya Kigeni wa Marekani Mike Pompeo anatazamia kukutana na afisa wa juu kutoka Korea kaskazini mjini New York katika mazungumzo yaliyolenga kuandaa mkutano muhimu kati ya marais wa mataifa hayo mawili.

Matangazo ya kibiashara

Kim Yong Chol, anayetajwa kuwa mshirika muhimu wa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un, alikuwa afisa wa juu wa taifa hilo kuwahi kuzuru taifa la Marekani katika kipindi cha miaka 18.

Vikao vingine viwili kati ya maafisa wa mataifa hayo mawili vimepangwa kufanyika alhamisi wiki hii.

Hiki ni kikao cha tatu kati ya maafisa hawa wawili ambao wanashughulikia hitimisho la maandalizi ya mkutano adhimu wa June 12 uliokusudia kumaliza mzozo wa nyuklia ambao ulitishia kusababisha vita katika rasi ya Korea.

Afisa mmoja wa Marekani amesma wawili hao wanakutana kuhakikisha mahitaji gani yanatakiwa kufanyiwa kazi ndani ya majuma mawili yaliyobaki kabla ya mkutano huo wa Trum na Kim.