CHINA-MAREKANI-TAIWANI-USHIRIKIANO

China yaitahadharisha Marekani juu ya suala la Taiwan

Rais wa Marekani Donald Trump na kiongozi wa China Xi Jinping (kulia) wakikutana kando ya mkutano wa nchi zilizostawi kiuchumi (G20) Hamburg, Ujerumani, Julai 8, 2017.
Rais wa Marekani Donald Trump na kiongozi wa China Xi Jinping (kulia) wakikutana kando ya mkutano wa nchi zilizostawi kiuchumi (G20) Hamburg, Ujerumani, Julai 8, 2017. ©REUTERS/Saul Loeb, Pool/File Photo

Serikali ya China imeitolea wito Marekani kuchukua hatua kwa uangalifu juu ya suala la Taiwan ili kuepuka uhasama katika uhusiano kati ya nchi hizi mbili na mdororo wa usalama katika eneo la Taiwan.

Matangazo ya kibiashara

Wakati ambapo maafisa wa Marekani waliliambia shirika la habari la Reuters kuwa watatuma meli za vita kupiga doria kwenye maji yanayotenganisha Taiwan na China Bara, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa China, Hua Chunying, amesema Beijing inachukulia Taiwan kama "sababu muhimu zaidi na nyeti" katika uhusiano wake na Washington.

"Marekani inapaswa kushughulikia kwa uangalifu suala la Taiwan ili kuepuka kuharibu uhusiano kati ya nchi hizi mbili (China na Marekani) na utulivu katika eneo la Taiwan," amesema msemaji huyo akitoa wito kwa Marekani kuheshimu "kanuni ya China moja" ".

Uhusiano kati ya China na Taiwan uliharibika tangu ushindi wa mgombea anayetetea kujitenga kwa eneo la Taiwan, Tsai Ing-wen, katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2016.

Meli za kivita za China zilikua zikipiga kambi na kupiga doria katika eneo hilo la Taiwan.

China na Marekani pia ziliendelea katika miezi ya hivi karibuni na mazoezi ya kijeshi ya pamoja ya baharini karibu na visiwa vilivyojitenga na China katikati Bahari ya Kusini mwa China.

China na Marekani zikifanya mazoezi ya kijeshi ya pamoja katikati Bahari ya Kusini mwa China Mei 11, 2018.
China na Marekani zikifanya mazoezi ya kijeshi ya pamoja katikati Bahari ya Kusini mwa China Mei 11, 2018. Handout / TAIWAN DEFENCE MINISTRY / AFP