THAILAND-USALAMA

Njia bora ya kuwaokoa wavulana 12 na kocha wao yatathminiwa thailand

Waokoaji nchini Thailand kwa sasa wanatathmini njia iliyo bora zaidi watakayotumia kufanikisha kuwaokoa wavulana 12 na kocha wao waliokwamba katika pango hadi seheme ya usalama.

Wavulana 12 walio na umri ulio chini ya miaka 16 na kocha wao wanasubiri kuokolewa baada ya kukwama katika pango.inside a flooded cave in Chiang Rai, Thailand, July 3, 2018, in this still image taken from a Thai Navy Seal handout video.
Wavulana 12 walio na umri ulio chini ya miaka 16 na kocha wao wanasubiri kuokolewa baada ya kukwama katika pango.inside a flooded cave in Chiang Rai, Thailand, July 3, 2018, in this still image taken from a Thai Navy Seal handout video. ©hai Navy Seal Facebook/Handout via Reuters
Matangazo ya kibiashara

Waokoaji nchini Thailand wanasema, hawatalazimika kuhatarisha maisha ya wavulana hao kocha wao, waliokwama ndani ya handaki kwa zaidi ya siku 10 sasa.

Wavulana hao wamepokea chakula kwa mara ya kwanza pamoja na dawa, baada ya waokoaji kufika katika handaki hilo.

Watalaam kutoka mataifa mbalimbali kwa sasa wanaendelea kuthathmini namna ya kuwaokoa, huku maombi yakiwa kuwa mvua kubwa haitaendelea kunyesha na kutatiza juhudi za kuwaokoa.

Wachezaji hao walikwenda kwenye handaki hilo kufanya mazoezi lakini, viwango vya maji viliongezeka na hivyo wakashindwa kuondoka.

Mvua nyingi zinazonyesha zinaashiria kiwango cha maji kujaa na kuhatarisha maisha ya watu waliomo pangoni pamoja na mifuko ya hewa waliyonayo mahali waliko kama mateka.

Wavulana hao waligunduliwa siku tisa baada ya kuingia pangoni humo huko katika jimbo la Chiang Rai kufuatia mafunzo ya mpira waliyokuwa wakifanya na kujikuta wakikwama pangoni kutokana na kina cha maji kuongozeka kulikosababisha na mvua nyingi zinazonyesha.