JAPANA-MAJANGA YA ASILI

Watu zaidi 100 wafariki dunia kufuatia mvua zinazonyesha Japan

Wakaazi wa mji wa Stricken, Japan, ulioathirika na mafuriko, Julai 9, 2018.
Wakaazi wa mji wa Stricken, Japan, ulioathirika na mafuriko, Julai 9, 2018. © AFP

Jumatatu wiki hii waokoaji wamekuwa wakijaribu kutafuta watu waliotoweka katika vitongoji vilivyofunikwa na matope na katika vifusi vya nyumba, magharibi mwa Japan ambapo watu zaidi ya 100 wamefariki baada ya mvua kubwa kunyesha.

Matangazo ya kibiashara

Waziri Mkuu, Shinzo Abe, ameamua kufuta ziara yake katika nchi nne kuanzia Jumatano huko Ubelgiji, Ufaransa, Saudi Arabia na Misri ili kutoa kipaumbele kwa waathirika, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Japan.

Kwa mujibu wa chanzo cha hospitali, watu 87 wamefariki dunia na 13 wako katika hali mbaya ya kusimama kwa mapigo ya moyo na kupumua. amesema Jumatatu wiki hii msemaji wa serikali, Yoshihide Suga, wakati mkutano na vyombo vya habari.

Katika jiji la Kumano, maporomoko makubwa ya udongo yameteketeza nyumba kadhaa, waandishi wa habari wa shirika la habari la AFP wamebaini.