MAREKANI-CHINA-USALAMA

Mlipuko mkubwa watokea nje ya Ubalozi wa Marekani Beijing

Mlipuko mkubwa umesikika Alhamisi wiki hii huko Beijing mbele ya Ubalozi wa Marekani, mashahidi meandika kwenye mitandao ya kijamii.

Mlipuko umemjeruhi mtu mmoja, ambaye alikua akijaribu kuchoma moto kifaa cha kulipuka. Picha ya kumbukumbu.
Mlipuko umemjeruhi mtu mmoja, ambaye alikua akijaribu kuchoma moto kifaa cha kulipuka. Picha ya kumbukumbu. NICOLAS ASFOURI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Picha na video ambazo zimerushwa kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha moshi mkubwa ukifumba nje ya jengo la Ubalozi wa Marekani.

Hata hivyo Ubalozi wa Marekani nchini China umejizuia kusema chochote kuhusiana na hali hiyo.

Lakini chanzo cha serikali ya China kilio kuwa karibu na eneo la tukio kimethibitisha tukio hilo.

Kwa mujibu wa polisi, mlipuko huo umesababishwa na mtu ambaye amejeruhiwa akijaribu kulipua kifaa  hicho.

Mtu huyo mwenye umri wa miaka 26 kutoka Mkoa wa Mongolia amelazwa hospitali, na anaendelea vizuri, polisi ya China imesema katika taarifa yake, ikiongeza kuwa hakuna mtu mwingine aliyejeruhiwa katika mlipuko.