UTURUKI-HAKI

Mahakama ya Uturuki yaagiza kuachiliwa huru kwa kiongozi wa Amnesty

Mahakama ya Uturuki imeamua kumwachilia huru kwa dhamnakiongozi wa Amnesty International nchini humo, Taner Kilic.
Mahakama ya Uturuki imeamua kumwachilia huru kwa dhamnakiongozi wa Amnesty International nchini humo, Taner Kilic. REUTERS/Leonhard Foeger

Mahakama ya Uturuki imeamuru kuachiliwa huru kwa kiongozi wa shirika la kimataifa la Haki za Binadamu la Amnesty International nchini humo, Taner Kilic, Mwanaharakati wa shirika moja la haki za binadamu amesema.

Matangazo ya kibiashara

Taner Kilic alishtakiwa kuunga mkono mhubiri aliyeuhamishoni Fethullah Gulen, ambaye Ankara inamhusika na jaribio la mapinduzi lililoshindwa Julai 2016.

Hajatolewa gerezani bado, mtafiti wa Amnesty International AI Andrew Gardner ameliambia shirika la habari la Reuters.

Uturuki imewakamata wanasiasa wengi wa upinzania pamoja na askari, polisi na wafanyakazi wengine wa serikali.