Familia za watu kutoka Korea Kaskazini na Kusini zakutana kwa mara ya kwanza

Raia wa Korea Kusini wakishiriki mkutano wa kifamilia kabla ya kufanya safari kukutana na ndugu zao Korea Kaskazini Agosti 19, 2018.
Raia wa Korea Kusini wakishiriki mkutano wa kifamilia kabla ya kufanya safari kukutana na ndugu zao Korea Kaskazini Agosti 19, 2018. Ed JONES / AFP

Familia kadhaa za raia wa Korea Kaskazini na Kusini zilizotenganishwa na vita zimekutana kwa mara ya kwanza. wengi mwa watu hao ni wazee ambao kwa sasa wana umri mkubwa. Watu hao walitengana miaka 70 iliyopita, baada ya vita kuzuka kati ya mwaka 1950-1953

Matangazo ya kibiashara

Familia nyingi zilitengana wakati wa vita hivyo, vilivyosabisha Korea kugawanywa mara mbili.

Hii ndio mara ya kwanza kwa kipindi cha miaka mitatu, familia ya wazee hawa walio na umri wa hadi kufikia 101 wakikukutana na wapendwa wao.

Hatua hii inakuja miezi michache baada ya Rais Moon Jae-in kukutana ana kwa ana na rais Kim Jong-un kwenye mpaka kati ya nchi hizo mbili, siku ya Ijumaa.

Mzungumzo hayo ya kihistoria yalelenga nia ya hivi karibuni ya Korea Kaskazini ya kuachana na silaha za nuklia.

Mkutano huo wa tatu baada ya mkutano wa mwaka 2000 na 2007 ni matokeo ya jitihada zilizofanyika miezi kadhaa kuimarisha mahusiano kati ya Korea hizi mbili na kufungua milango ya mkutano kati ya Kim na Rais wa Marekani Donald Trump.