BURMA-VYOMBO VYA HABARI-HAKI

Waandishi wawili wa habari wahukumiwa kifungo cha miaka 7 Burma

Muda mfupi baada ya uamuzi wa Mahakama, Septemba 3. "Waandishi hawa wawili wa habari wamezuiliwa miezi tisa jela kwa shutma za uongo ili kuvinyamazisha na kuvifavyia vitisho vyombo vya habari," shirika la Habari la Reuters limebaini.
Muda mfupi baada ya uamuzi wa Mahakama, Septemba 3. "Waandishi hawa wawili wa habari wamezuiliwa miezi tisa jela kwa shutma za uongo ili kuvinyamazisha na kuvifavyia vitisho vyombo vya habari," shirika la Habari la Reuters limebaini. REUTERS/Ann Wang

Waandishi wawili wa habari wa shirika la Habari la Reuters, wamehukumiwa kifungo cha miaka saba nchini Burma. Wakati huo huo Umoja wa Mataifa umeomba waandishi hao wa habari waachiliwe huru mara moja.

Matangazo ya kibiashara

Waandishi hao wa habari, Wa Lone na Kyaw Soe Oo, wanashutumiwa "kuvunja Sheria Rasmi ya Siri" kwa kuchunguza mauaji ya watu kutoka jamii ndogo ya Waislamu wa Rohingya, mauaji yaliyotekelezwa na jeshi la Burma.

Kesi hii imechafua jina la mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel, Aung San Suu Kyi. "Tunaendelea kuomba waachiliwe huru," Ostby Knut, mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini Burma, ameliambia shirika la Habari la AFP.

Mbele aya umati watu ikiwa ni pamoja na waandishi wa habari na wadiplomasia waliokuja kusikiliza uamuzi wa mahakama, Jaji Ye Lwin amesema Wa Lone, mwenye umri wa miaka 32, na Kyaw Soe Oo, mwenye umri wa miaka 28, ambao wanashikiliwa tangu mwezi Desemba 2017, " wote walivunja Sheria Rasmi ya Siri, na wanahukumiwa kila mmoja kifungo cha miaka saba.

Waandishi hawa wa habari wanashutumiwa kupata nyaraka zinazohusiana na operesheni za vikosi vya usalama vya Burma katika Jimbo la Rakhine, eneo la kaskazini magharibi mwa Burma, ambako kulitokea mauaji makubwa ya watu kutoka jamii ndogo ya Waislamu wa Rohingya. Walikuwa wakichunguza mauaji dhidi ya watu kutoka jamii ya Rohingya katika kijiji cha Inn Dinn. Siku chache baada ya kukamatwa kwao, jeshi lilikiri kwamba askari na wanakijiji wa Kibudha waliua watu kutoka jamii ya Rohingya mnamo Septemba 2, 2017, na askari saba walihukumiwa miaka kumi jela kwa mauaji hayo.

Hukumu hii inatolea katika hali ya mvutano mkubwa kati ya Burma na jumuiya ya kimataifa: wiki iliyopita, wachunguzi wa Umoja wa Mataifa walichapisha ripoti ya kubani kwamba kulitokea "mauaji ya kimbari" kwa jamii ya Rohingya na kulishumu moja kwa moja jeshi la Burma. Jumanne iliyopita, suala la kufunguliwa mashtaka askari waBurma katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu lilijadiliwa katika kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Mnamo Septemba 1, huko Yangon, mamia ya waandamanaji waliomba kuachiliwa huru kwa waandishi hao wawili wa habari, wakisisitiza kuhusu uhuru wa vyombo vya habari. Mwaka 2017, zaidi ya watu 700,000 kutoka jamii yaRohingya walikimbilia Bangladesh kutokana na unyanyasaji uliokua ukiendeshwa na vikosi vya jeshi vya Burma na wanamgambo wa Kibudha.