Japan yawataka raia wake kuhama baadhi ya maeneo kufuatia kimbunga Jeba

Bandari ya uvuvi huko Aki, magharibi mwa Japan.
Bandari ya uvuvi huko Aki, magharibi mwa Japan. REUTERS/Kyodo

Mamlaka ya Japan imetoa maelekezo ya kuhamishwa kwa wakazi karibu 300,000 na kufutwa kwa safari za ndege zaidi mia moja wakati dhoruba kali inayofahamika kwa jina la Jebi ikitarajia kupiga katika maeneo kadhaa ya nchi hiyo leo Jumanne.

Matangazo ya kibiashara

Jebi ni dhoruba kali zaidi ambayo imekua ikikumba Japan tangu mwanzoni mwa majira ya joto, wakati katika miezi ya hivi karibuni nchi hiyo ilikumbwa na majanga mengi ya asili kama vile mvua yenye upepo mkali, vimbunga, maporomoko ya ardhi, mafuriko na joto kali - ambavyo vilisababisha mamia ya watu kupoteza maisha.

Dhoruba hii inatarajiwa kuanza kupiga huko Shikoku, kisiwa kidogo kati ya visiwa vinne vikuu nchini Japan, kabla ya kupiga Honshu, kisiwa kikuu, huko Osaka, kisiwa cha pili kwa ukubwa nchini humo.

Mamlaka imewataka watu 280,000 kuhama makaazi yao, wakati upepo na mvua zimeanza kujikusanya.

Safari za ndege karibu 600 zimeutwa, ikiwa ni pamoja na safari za majini, televisheni ya serikali NHK imeripoti.

Mji mkuu, Tokyo, hautokubwa na dhoruba hii lakini kunatarajiwa kunyesha mvua kubwa na upepo mkali mwishoni Jumanne jioni.