URUSI-JAPAN-USHIRIKIANO

Putin apendekeza mkataba wa amani na Japan

Rais wa Urusi Vladimir Putin, pamoja na Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe, Septemba Vladivostok.
Rais wa Urusi Vladimir Putin, pamoja na Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe, Septemba Vladivostok. ALEXEI DRUZHININ / SPUTNIK / AFP

Rais wa Urusi Vladimir Putin amewashangaza wengi Jumatano wiki hii kwa kutoa pendekezo kwa Japan kufunika ukurasa wa Vita Kuu vya Pili vya Dunia na kutiliwa saini mkataba wa amani. 

Matangazo ya kibiashara

Rais Putin amesema angelifurahi nchi hizi mbili kutia saini mkataba wa amani mwaka huu "bila masharti".

Rais wa Urusi ametoa pendekezo hilo katika mkutano wa kiuchumi huko Vladivostok, Mashariki mwa Urusi, ambapo Waziri Mkuu wa Japani Shinzo Abe alitoa wito mpya wa kutiliwa saini mkataba huo, mada kuu ya mazungumzo katika miaka ya hivi karibuni kati ya Moscow na Tokyo.

"Ni miaka 70 tangu tumejaribu kutatua tofauti zetu, ni miaka 70 tangu tumezungumza, " Shinzo amasema, huku akiongeza "tubadilishe mtazamo!

" Kwa uhakika: tufanye hivyo! Tutie saini mkataba wa amani ifikapo mwishoni mwa mwaka bila masharti yoyote",' amesema Vladimir Putin.

Taarifa hii inatofautiana na kauli ya hivi karibuni ya kiongozi wa Kremlin juu ya suala hili wakati wa mikutano ya hivi karibuni na Shinzo Abe. Alitoa wito mnamo mwezi Mei wa kuwa na "subira" na kusema tena siku ya Jumatatu kuwa itakuwa "vigumu kufikiri kwamba mgogoro huu unaweza kutatuliwa kwa saa moja.

Uhusiano kati ya Moscow na Tokyo ulidorora kutokana na uhasama kuhusu visiwa vinne vya rasi ya Kurile iliyodhibitiwa na Urusi mwishoni mwa Vita Kuu vya Pili vya Dunia. Japan inasema kuwa visiwa hivi ni sehemu yake na mgogoro huu hadi sasa umezuia nchi hizi mbili kutia saini mkataba wa amani.