UFILIPINO-MAJANGA YA ASILI

Thelathini wafariki dunia kufuatia kimbunga Magnkhut Ufilipino

Waokoaji kutoka Ufilipino waendelea kutafuta watu walifunikwa na matope baada yakimbunga Mangkhut kupiga Baguio, Septemba 16, 2018.
Waokoaji kutoka Ufilipino waendelea kutafuta watu walifunikwa na matope baada yakimbunga Mangkhut kupiga Baguio, Septemba 16, 2018. REUTERS/Harley Palangchao

Kimbunga Magnkhut kimeua watu thelathini na wengine kadhaa hajulikani walipo kaskazini mwa Ufilipino. Zoezi la kuwatafuta watu waliokwama chini ya vifusi baada ya kufunikwa na matope linaendelea. Lakini vyanzo kadhaa vinasema hakuna matumaini ya kwapata hai watu hao.

Matangazo ya kibiashara

Hali hii imesababishwa na mvua nyingi zilizokua zikinyesha juma lililopita katika eneo mwa kaskazini la Ufilipino.

Kwa mujibu wa mashirika ya kihisani, familia takriban 26,367 zilizoathirika katika eneo hilo zinahitaji msaada wa chakula na mahitaji mengine.

Wengi wa wakaazi wa eneo hilo walikumbwa na maporomoko ya udongo yaliyosababishwa na mvua kubwa.

Baadhi ya maeneo ya kisiwa cha Luzon yamekumbwa na mafuriko, yakiwemo mashamba ya mpunga na mahindi ambayo huzalisha mazao makuu nchini humo.

Jumapili mchana Rais Rodrigo Duterte alizuru mkoa wa Cagayan, kaskazini mwa nchi hiyo, ambako kimbunga Mangkhout kilipiga na kuathiri maeneo maengi. Nyumba nyingi ziliathirika, na watu wengi walitakiwa kuhama na kwenda maeneo salama, huku watu 100,000 pekee walihamishwa kutoka kisiwa cha Luzon.