KOREA KASKAZINI-KOREA KUSINI-ZIARA

Rais wa Korea Kusini azuru Korea Kaskazini, apokelewa kwa shangwe

Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in amezuru jijini Pyongyang nchini Korea Kaskazini anakokutana na kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong Un.

Rais wa Korea Kusini  Moon Jae-in akikaribishwa na mwenyeji wake Kim Jong Un, Septemba 18 2018 jijini Pyongyang
Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in akikaribishwa na mwenyeji wake Kim Jong Un, Septemba 18 2018 jijini Pyongyang Pyeongyang Press Corps/Pool via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Ziara ya Moon inalenga kuendeleza mazungumzo na serikali ya Korea Kaskazini kuhusu kuachana kabisa na mpango wake wa kutengeneza silaha za nyuklia na kuimarisha uhusiano wake na Marekani.

Baada ya kuwasili, rais Moon alitembezwa katikati ya jiji la Pyongyang na kusalimiwa na maelfu ya raia wa nchi hiyo waliojitokeza kwa wingi kumwona.

Kabla ya ziara hiyo katikati ya Pyongyang, Kim Jong UN, alikwenda kumpokea katika uwanja wa Kimataifa wa ndege.

Mbali na mazungumzo ya nyuklia, tangu kuingia madarakani, rais Moon amekuwa akijitahidi sana kuimarisha uhusiano wa mataifa hayo jirani.

Korea Kusini na Kaskazini ilitenganishwa wakati wa vita kati ya nchi hizo mbili miaka 1950.