MAREKANi-IRAn-ICJ-HAKI

Mahakama ya kimataifa kutoa umuzi wake kuhusu vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran

Aprili 2 mwaka 2015, katika mji wa Lausanne, Uswisi, makubaliano ya kisiasa yakifikiwa kati ya Tehran na mataifa yenye nguvu duniani kuhusu suala la mpango wa nyuklia wa Iran.
Aprili 2 mwaka 2015, katika mji wa Lausanne, Uswisi, makubaliano ya kisiasa yakifikiwa kati ya Tehran na mataifa yenye nguvu duniani kuhusu suala la mpango wa nyuklia wa Iran. REUTERS/Ruben Sprich

Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) inatarajia kutoa uamuzi wake Jumatano wiki hii kuhusu ombi la Tehran la kusitishwa kwa vikwazo vya Marekani vilivyowekwa na Donald Trump. Iran imelaani vikwazo hivyo ikisema kuwa vina madhara makubwa kwenye uchumi wake.

Matangazo ya kibiashara

Mahakama hiyo ya kimataifa, yenye makao yake makuu mjini Hague na ambayo ni mahakama ya juu ya Umoja wa Mataifa, itatoa uamuzi wake katika kikao cha hadhara kitakachoanza saa 10:00 (sawa na saa 8:00 saa za kimataifa).

Uamuzi wa ICJ unakuja katika hali ambapo mvutano kati ya Iran na Marekani umeongezeka, na hivi karibuni marais wa Irani na Marekani walitupiana vijembe katika Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa wiki iliyopita.

Mnamo mwezi Mei Rais wa Marekani aliiondoka nchi yake kwenye mkataba wa nyuklia uliyotiliwa saini mwaka 2015. Marekani, Iran na mataifa yenye nguvu duniani zilitia saini kwenye mkataba huo.