MAREKANi-IRAN-ICJ-HAKI

ICJ yaitaka Marekani kusitisha vikwazo dhidi ya Iran

Mahakama ya Kimataifa ya Haki imeitaka Marekani kusitisha vikwazo vya aina yoyote  vinavyohusiana na dawa, vyakula na vifaa vya magari na ndege kwenda Iran.
Mahakama ya Kimataifa ya Haki imeitaka Marekani kusitisha vikwazo vya aina yoyote vinavyohusiana na dawa, vyakula na vifaa vya magari na ndege kwenda Iran. STRINGER / afp

Marekani imesitisha mkataba wake na Iran wa mwaka 1955 ulioruhusu nchi hizo mbili kwenda katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) kutatua tofauti zozote katika ya nchi hizo mbili.

Matangazo ya kibiashara

Iran imekuwa ikilaani vikwazo hivyo ikisema kuwa vina madhara makubwa kwenye uchumi wake.

Hatua hii imekuja baada ya Majaji 15 wa Mahakama hiyo kwa kauli moja, kuamua kuwa Marekani isitishe vikwazo dhidi ya Iran ambavyo ni pamoja na kuzuiwa kwa dawa, vyakula na vifaa vya magari na ndege kwenda katika nchi hiyo.

Marekani imelaani hatua hiyo ya Mahakama huku Iran ikishangilia.

Uamuzi wa ICJ unakuja katika hali ambapo mvutano kati ya Iran na Marekani umeomgezeka, na hivi karibuni marais wa Irani na Marekani walitupiana vijembe katika Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa wiki iliyopita.

Rais wa Mahakama hiyo Abdulqawi Ahmed Yusuf ameonya pande zote kuacha kufanya chochote kitakachosabisha mzozo zaidi.

Hata hivyo Mahakama hiyo haina uwezo wowote ili kupelekea hatua yake iweze kutekelezwa.

Mnamo mwezi Mei Rais wa Marekani aliiondoka nchi yake kwenye mkataba wa nyuklia uliyotiliwa saini mwaka 2015. Marekani, Iran na mataifa yenye nguvu duniani zilitia saini kwenye mkataba huo.